MACHUMU, ANG'ATUKA TEF, MGONGANO WA MASLAHI WA WADHIFA NDIO CHANZO.
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline
DAR ES SALAAM
MKURUGENZI wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu amejijuzulu nafasi ya makamu mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa kile alichodai kwa nafasi yake mpya anaona kutakuwa na mgongano wa masilahi na wadhifa huo.
Machumu ambaye hivi karibuni ameteuliwa na Rais Dtk.Samia Suluhu Hassan kuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu amekabidhi barua ya kujiuzulu kwake kwa Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, leo Novemba 26, 2025 alipokutana na wahariri kwenye kikao cha ndani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile amepokea baruahi hiyo na kukubali kujiuzulu kwa Machumu na kuwa Kamati ya Utendaji ya TEF itakutana baadaye leo kujadili suala hilo.

Comments
Post a Comment