CHINA NA TANZANIA KUBORESHA RELI YA TAZARA KWA KIWANGO CHA SGR.

  Timothy Marko DmNews online 

             DAR ES SALAAM.

BALOZI  wa China Nchini Tanzania Chen Mingjian amesema itaendelea Kudumisha Mahusiano ya Uchumi wa kikanda kati yake na Tanzania na Zambia katika kuboresha Sekta ya Miundombinu ikiwemo reli ya Tazara.

Akizungumza Katika hafla ya makubaliano ya Ujenzi wa reli ya Tazara kwa kiwango cha Kimataifa SGR, Balozi Chen Mingjian amesema kuwa China ni mdau Muhimu wa Maendeleo kati ya Tanzania na Zambia kupitia reli ya Tazara.
,,
Ilikuweza kuhakikisha Sekta ya Bandari inaimarika Sekta ya Miundombinu ya reli nimuhimu kuboreshwa kwa kiwango cha Kimataifa,, Amesema Chen Mingjian.

Mingjian Ameongeza kuwa uboreshwaji wa Sekta ya Bandari kutawezesha Uchumi wa Nchini ambazo Hazina Bandari kukuwa .
Ameongeza kuwa uboreshwaji wa reli hiyo yenye Umri wa miaka 50 utawesha Uchumi wa Tanzania na Zambia.kukuwa 
,,
Wazo lauboreshaji wa reli ya Tazara kwa kiwango cha Kimataifa SGR liibuliwa na Rais wa Zambia Hechilema alipokutana na Makamu wa Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Emanuel Nchimbi alipoitembelea Nchi ya Zambia hivi karibuni ,, Amebainisha Balozi wa china Nchini Tanzania Chen Mingjian.

Aidha, kwaupande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Ashatu Kijaji amesema kuwa Ushirikiano wa Tanzania na Zambia Pamoja na China Unalenga kuboresha Sekta ya Miundombinu ya Reli ikiwemo SGR.

Amesema kuwa Shiriakiano wa china na Tanzania ni wakipindi kirefu Ambapo amesema uboreshwaji wa Reli ya Tazara kwa kiwango cha Kimataifa SGR utaenda Sambamba na Maboresho ya Bandari ya Tanga.
,,
Uhusino huu kati ya Nchi za China na Tanzania ni wa Enzi na Enzi wa Kabla ya Uhuru na Baada ya Uhuru,, Alibainisha Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Ashatu Kijaji.   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.