MJUMBE WA KAMATI YA SIASA MKOA WA PWANI DKT. TINDWA ATOA UJUMBE NZITO UFUNGAJI KAMPENI KISARAWE

 Na Mwandishi wetu,DmNewsonline

            KISARAWE 


MJUMBE wakamati ya Siasa Mkoa Pwani Dkt  Chakou Tindwa Amewaeleza watanzania na wananchi wa kata ya Makurunge wilaya ya kisarawe kwamba waendelee kukuamini Chama Cha Mapinduzi CCM kwani kinafanya kazi kubwa ya kuwaletea Maendeleo.

Dkt Tindwa ameyasema hayo leo Octoba 26, 2025 wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi ngazi ya Ubunge Jimbo la kisarawe ambapo amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi ukiangalia katika upande wa miundombinu ya Barabara ,afya ,umeme, shule ,maji utaona kwamba Kuna kazi kubwa imefanyika .

Amesema ifike wakati kuachana na porojo ambazo zinasemwa na watu wasiolitakia mema Taifa badala yake wapime wenyewe kazi hizo ambazo zinafanywa na viongozi thabiti wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi CCM.

Amesema mambo yanayofanyika katika maeneo hayo ambayo ameyataka utagundua kuwa Tanzania IPO juu ya majirani wanaoizunguka nchi na unaweza kuthibitisha hayo kwa kuangalia takwimu na si maneno maneno tu ya kwenye mitandao .

"Ilituweze kupata kura za kutosha basi hakikisha wewe najira zako wote mnatoka kwenda kupiga kura na kukichagua Chama Cha Mapinduzi CCM "amesema Dkt Tindwa 

CCM na viongozi wake tunania nzuri na thabiti ya kulipeleka Taifa hili mbele kwa kutekeleza yale ambayo yameelekezwa kupitia Ilani yake  nyie mnatambua hilo  ndio maana tunasema twendeni mkakichague Chama Cha Mapinduzi CCM ."amesisitiza Dkt Tindwa 

Naye Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM Jimbo la kisarawe Alhaj Dkt Selelman Jafo amewaomba wananchi wa jimbo hilo kwenda kupiga kura ifikapo Octoba 29,2025 .

Amesema kuwa kutokana na kazi kubwa ambazo amezifanya Mgombea urais wa Chama hicho Dkt Samia Suluhu Hassan Ikiwepo kazi ya kuleta miradi mingi ya maendeleo Jimbo la kisarawe shukrani yake ni kwenda kumpigia kura nyingi .

Dkt Jafo ameyasema hayo katika mkutano wa kufunga kampeni jimboni humo, wananchi jitokezeni kwa wingi wenu umoja wenu kwenda kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi CCM

Mwenyekiti wa Kamati ya ushindi kanda ya Mashariki Sophia Simba  awali akimnadi Mgombea huyo ubunge amewataka wananchi hao kuwa Octoba 29 mwaka huu hakuna kufanya makosa kwani ndio siku mwali anatoka huku akiwataka Kila mtu kutoka na mwezake .

Amesema kwa mara ya Kwanza nchi inakwenda kupata Mgombea mwanamama  na Kwa kazi aliyofanya tafasili yake inatakiwa apate kura nyingi zaidi na kisarawe mara nyingi hamfanyi makosa.

Mstaafu huyo wa UWT Taifa amesema kwa mambo ambayo Dkt Samia amefanya inatakiwa wananchi wakampe zawadi  kubwa kwenye sanduku la kura, Dkt. Samia ametembea nchi nzima kwa ajili ya Kuomba kura.

" Tulimsikia akiwa katika uzinduzi pale kawe ahadi zake zipo wasiwazi na katika siku 100 za mwanzo  anakwenda kuondoa kero na anakwenda kutoa mikopo mengi kwa makundi mbalimbali ya vijana hivyo madiwani wawekeni vijana na hata wazee mkao wa kupata mikopo ."amesema

Naye katibu  wa Kamati ya  kimkakati ya  ushindi kanda ya Mashariki Hawa Ghasia amesema katika watu wanaogombea Urais hakuna anayekaribia sifa alizonazo Mgombea wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani anaozoefu wakazi anayomba ya Urais.

Amesema Dkt.samia ametumika kwa miaka minne na wengine uzoefu wao nikulala gerezani ,maandamano ,matusi lakini Dkt Samia amejenga zahanati , hospitali za kanda   Barabara za kutosha , ameendeleza kilimo na mambo mengine mengi.

Amewataka wananchi wamchague Dkt. Samia na ubunge wamchague Dkt Jafo kwani kero zenu atazipeleka kule taifani na pia mchagueni diwani wa kata ya kiluvya wakili Aidan kitale na changamoto za kiluvya atazipeleka kwa Dkt jafo nendeni mkawachague viongozi wanaotokana na CCM .   



Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.