MASANINGA : DKT. SAMIA AMEFANYA KAMPENI ZA KIUNGWANA MATARAJIO YA USHINDI NI MAKUBWA.

 Na Mwandishi wetu,DmNewsonline 

                    MKURANGA 

MGOMBEA udiwani wa kata ya kiparang,anda wilaya ya mkuranga  Mariam Masaninga ametumia siku ya leo kutoa pongezi zake za dhati kwa mgombea nafasi ya  Rais Dkt. Samia  Suluhu Hassan kwa kufanikisha kumaliza kampeni zake kwa amani na utulivu mkubwa 

Masaninga amesema kuwa Mgombea huyo wa Urais ameweza kuzunguka Nchi nzima kwa kufanya kampeni zake na hatimaye leo kufikia tamati.

Masaninga ameyasema hayo leo Oktoba 28 2025.Wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM kata ya kiparang,anda ambapo amesema kuwa mbali na kumpongeza Mgombea urais wa CCM lakini pia anamshukuru Mungu kwa kumaliza salama kampeni zake.

Amesema kuwa ili kuwa ni miezi miwili ya mchakamchaka  hekaheka lakini leo tunamshukuru Mungu kwa kufikia tamati leo na matarajio ni makubwa mno kupata ushindi  wa kishindo kabisa 

Pia Masaninga amesema kuwa anaimani kubwa mno na wananchi wa kiparang'anda kwamba wameshafanya maamuzi na Oktoba 29 ,2025 wanakwenda kutiki kwa Chama Cha Mapinduzi CCM.

Ameongeza kuwa wananchi wa Jimbo la mkuranga na vitongoji vyake wanaimani na viongozi wao akiwemo Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega kipekee Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

"Naomba sana wananchi wa mkuranga hasa kata kiparang'anda msifanye makosa naamini tumepita kote na tumezungumza mengi mno ya kuhusu Maendeleo lakini Imani yetu mnakwenda kukichagua Chama Cha CCM ."amesema 

Amefafanua kuwa kwa mara ya kwanza nchi yetu inakwenda kupata Rais mwanamke wa kuchaguliwa na wananchi wenyewe na Kwa kazi kubwa aliyoifanya ikiwemo ya kuzunguka Nchi nzima Kuomba kura na kunadi Ilani ya CCM niwazi Chama kinakwenda kupata ushindi wa mkubwa sana.

Masaninga amesema  kuwa mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa diwani wa kata ya kiparang'anda  kazi yake ya Kwanza nikwenda kujenga ofisi ya kata ya CCM kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo hilo  Alhaj Abdallah Ulega 

Mwisho amewaomba wananchi wa mkuranga  kujitokeza kwa wingi na Kwa umoja wao kwenda kupiga kura zote kwa Dkt.Samia  Suluhu Hassan,Alhaj Abdallah Ulega ,na yeye  Mariam Masaninga kuwa diwani wa kata ya kiparang,anda    

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.