MASANINGA, AHITIMISHA KAMPENI ZAKE KIJIJI ALICHOZALIWA MAGOZA MKURANGA

 Na Mwandishi wetu, DmNewsonline

             MAGOZA _MKURANGA


MGOMBEA Udiwani kata ya kiparang'anda wilaya ya  mkuranga mkoani Pwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM  Mariam Masaninga amewaomba wananchi wa Kijiji Cha magoza kuwa ifikapo Octoba 29, mwaka huu waenda kukipigia kura Chama hicho ili kiendelee kuwaletea Maendeleo .

Amewaeleza wananchi hao kuwa yeye kama mzaliwa wa Kijiji Cha magoza kata hiyo ya kiparang'anda anawaomba kwa moyo wa huruma kwenda kumpa kura Dkt .Samia Suluhu Hassan ,Mbunge wa Jimbo hilo   Alhaj ,Abdallah Ulega na yeye Mariama Masaninga kwa nafasi ya  diwani .
Masaninga ameyasema hayo leo Octoba  25, ,2025 alipokuwa anahitimisha kampeni za kuomba ridhaa ya wananchi wa Kijiji Cha magoza  katika nafasi ya Udiwani ili wamchague awe kiongozi wao kwa miaka mitano ijayo .

Mariam  amewaeleza wananchi hao dhamira ya dhati ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya kuendelea kuwatumikia watanzania na kuwaletea Maendeleo huku akibainisha kwamba kupitia Ilani ya uchaguzi ya 2025/30 imeeleza wazi miradi inayokwenda kutekelezwa katika Jimbo la mkuranga iliwepo kata ya kiparang'anda.

Amesema  rais Dkt.Samia amefanya kazi kubwa kwa miaka minne ya uongozi wake hivyo ili kuweza kumuonesha kama wako pamoja nae nikufanya maamuzi sahihi Octoba 29, mwaka huu kwa kuweza kumpigia kura za ndio kwneye sanduku la kura 

"Ndugu zangu nataka niwaambie kuwa yapo mengi yamefanywa chini ya Rais Dkt. Samia na Mgombea ubunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega kwa ushirikiano mkubwa na  Baraza la madiwani mkuranga twende tukaoneshe kwa kupiga kura nyingi kwa kiongozi wetu."amesema  

Masaninga amesema wanaomba kura ili waweze kuwa madiwani ili wakamalizie mambo yaliyobakia hasa kwenye upande wa maji ,Barabara , elimu , afya na kwamba yeye ameteuliwa na Chama hicho si kwamba yeye bora sana  ila ni utaratibu wa Chama lazima apatikane Mgombea mmoja .

"Niungeni mkono Mimi Mariam Masaninga kwa kunielekeza , na mnipe dhamana hii ili niende nikalekebishe pale ambapo panahitajika .naomba niwe kiunganishi wenu , kwa kusaidiana na Mgombea ubunge wa Jimbo la mkuranga ."amesema  Mariam

 zipo kero ambazo nimezichukua wakati nazunguka Kuomba ridhaa nakwamba changamoto za magoza zinakwenda kujibiwa na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ."

Ameongoza kuwa Ilani ya uchaguzi ya CCM  kwa wananchi wa mkuranga imetaja ukamilishaji wa zahanati , Barabara kiwango Cha changarawe kiparang'anda ,kibululu na kuhoji kuwa  hao wengine wataweza ?

Pia ununuzi wa madawati kwa shule za msingi  kiparang'anda , ujenzi wa shule za msingi kise  na magoza lakini ujenzi wa matundu kumi ya vyoo shule ya msingi kise ,magoza .na ukamilishaji wa nyumba za walimu sekondari ili watoto wapate elimu ya kutosha wakiwa na walimu wao hapo hapo kijijini magoza.

Pia amezungumzia mikakati na mipango ya kutekeleza miradi yote iliyoainishwa kupitia Ilani chama Cha Mapinduzi ikiwemo mikopo kwa makundi  mbalimbali wakiwemo vijana watu wenye ulemavu  wote wanakwenda kunufaika na mikopo hiyo .

Amewataka wananchi hao hususani vijana kwenda kuunda vikindu ili kuweza kupata mikopo hiyo inayotolewa na  halmashauri ya wilaya ya mkuranga lakini pia amezungumzia Mradi wa maji katika vijiji vya kata ya kiparang'anda na usamabazaji umeme kwenye vitongoji  na kiparang'anda vitongoji vyote vimeguswa.

Kwaupande wake sheikh wa kata ya kiparang'anda wilayani humo Sheikh  Abdarahman Kitando amewataka wananchi  wote wajitokeze kupiga kura kwa amani na Pasitoke mtu anashawishi wengine ili wasipige Kura.

 Kitando ameyasema hayo  baada ya kupewa nafasi ya kufanya Maombi kabla ya kuaza mkutano huo wa  kampeni za Udiwani kata ya kiparang'anda kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM .

Amesema hakuna jambo la muhimu na la msingi kama amani kwani ili uweze kufanya mambo yako ya kimaendeleo katika Mazingira yanayokuzunguka lazima amani na utulivu viwepo.

Katika mkutano huo wa kampeni Aliyekuwa meneja kampeni wa Chama Cha wananchi CUF  Mohamed Hamis aliweza kukabidhi kadi ya Chama Cha cuf na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM 

Akizungumza mara baada ya kujiunga na ccma Hamis amesema kuwa ameruf nyumbani baada kupotea kwa muda sasa amerudi sehemu yenye mafanikio hivyo amekwenda kuungana na timu ya ushindi CCM . 

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.