MGOMBEA URAIS KUNJE NA MGOMBEA MWEZA WAKE AAFP KUZINDUA KAMPENI KIHOMBOHOMBO MOROGORO AGOSTI 31
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
CHAMA cha Wakulima(AAFP) kinapenda kuwataarifu wananchi na wanachama wake,vyombo vya habari kuwa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 zitafanyika Kihombohombo Vijijini Mkoa wa Morogoro Agosti 31,,2025 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 12:00 Jioni
Katika uzinduzi huo,Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kunje Ng'ombale Mwiru pamoja na mgombea Mwenza Chumu Abdallah Juma wanatarajiwa kuhutubia wananchi na kueleza kwa kina sera na vipaumbele vya Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha AAFP kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.
Aidhaa ,viongozi wakuu wa chama,wagombea ubunge ,na wagombea wa udiwani kutoka mikoa mbalimbali nchini watashiriki katika tukio hilo kubwa la kihistoria na la kisiasa pamoja na wasanii mbalimbali wa bongo fleva watakupo
Wakazi wote wa Mkoa wa Morogoro na mikoa ya Jirani mnakaribishwa kuhudhuria kwa wingi katika uzinduzi huo wa kampeni ili kupata nafasi na fursa ya kusikiliza sera zinazolenga kuleta maendeleo ya nchi na kwa ustawi wa Mtanzania
Taarifa hii imetolewa kwa njia ya simu Leo Agosti 30,2025 na Naibu Mkuu wa AAFP Mark Isdory Mhemela akiwa sehemu ya tukio pia amewatakia Kila la heri wagombea wote wa AAFP nchi kushiriki kampeni za amani na utulivu.
Sanjari na hayo ,amesema katika kampeni hizo wapo wanachama wapya watakaojiunga na Chama hicho .

Comments
Post a Comment