SIGRADA MLIGO:NIMEONDOKA CHADEMA, KIMEKOSA MWELEKEO WA KUKIONDOA CCM MADARAKANI.
Timothy Marko DmNewsonoine
DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA KATIBU Mwenezi wa Baraza la Wanawake Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA SIGRADA MLIGO amesema Ameondoka Chama hicho na kujiunga na Chama cha Umma ,Baada ya CHADEMA kukosa Dhamira ya dhati ya kukiondoa Chama cha Mapinduzi CCM Madarakani
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam SIGRADA MLIGO amesema kuwa Chama cha Mapinduzi CCM Wana akiili ya Kisiasa,hivyo inahitaji jitihada za dhati za kuking'oa Chama hicho Madarakani.
"Ili Uweze kuking'oa Chama cha Mapinduzi CCM Madarakani lazima Ukifanye Chama cha Mapinduzi CCM kisilale " Amesema SIGRADA MLIGO.
MLIGO Ameongeza kuwa amekuwa akishutumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuwa anakihujumu Chama hicho.
Amesisitiza kuwa Amekuwa na Imani na Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lisu kuwania Urais lakini Kumekuwa na sitofahamu Juu ya Hatima yake.
"Nimekuja Chauma kuungana na kuungana na KATIBU Mkuu wa Chama cha Salumu Mwalimu tumekuwa wote Chuo, Nimependa Sera za Chama cha uuma" Amesema MLIGO. 

.

Comments
Post a Comment