MLAWA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA KILOLO _IRINGA
Na Eliasa Ally DmNewsOline I
RINGA
MDAU wa maendeleo na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Iringa, Aidan Mlawa, leo amechukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Kilolo kupitia chama hicho.
Hatua hiyo inamuweka rasmi katika kinyang’anyiro cha kusaka ridhaa ya wananchi kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho.
Mlawa, amejijengea heshima kubwa kwa mchango wake katika shughuli za kijamii, amekuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi wa Wilaya ya Kilolo hususani wale walioko kwenye mazingira magumu, pamoja na kushiriki kwa karibu katika kupigania utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 

Comments
Post a Comment