HINDU SENYANGE AJITOSA UDIWANI VITI MAALUMU SEGEREA
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Jumuiya ya Wazazi Kata ya Liwiti Segerea,Hindu Ally Senyange amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Udiwani wa Viti Maalumu Halmashauri ya Ilala.
Fomu hiyo amekabishiwa leo Juni 30,2025 na Katibu wa Umoja wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT)Wilaya ya Ilala ,Rosemary Mwakisalu
Aidha,Senyange amesema kwamba ameamua kugombea Udiwani wa Viti Maalum ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea watanzania maendeleo
Comments
Post a Comment