Posts

Showing posts from June, 2025

NDOSI BALAA ATUA KUCHUKUA FOMU YA KUWANIA UBUNGE WA JIMBO LA KIBAHA MJINI

Image
Na Mwandishi wetu,DmNews,Online,                         KIBAHA  MMOJA  wa Mwanachama wa chama cha  mapinduzi (CCM) amejitosa kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025.  Mgombea huyo ambaye anafahamika kwa jina la  Godwin Ndosi amesema ameamua kuchukua  fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kibaha Mji ili aweze kuendeleza pale alipoachia mwenzake Silvestry Koka. Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo  Ndosi amesema kuwa anatambua Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka amefanyakazi kubwa lakini na yeye anaingia kwa ajili ya kuendeleza pale ambapo Koka ameishia. "Nimekuja hapa kuchukua fomu na lengo kubwa ni kuleta mabadiliko ya Kibaha Mjini hususani katika kuwaletea Wananchi maendeleo lakini natambua Mbunge Koka kafanya mengi na mimi nitaendeleza pale alipoishia na lengo ni kuwalet...

HINDU SENYANGE AJITOSA UDIWANI VITI MAALUMU SEGEREA

Image
     Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline          DAR ES SALAAM  MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Jumuiya ya Wazazi Kata ya Liwiti Segerea,Hindu Ally Senyange amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Udiwani wa Viti Maalumu Halmashauri ya Ilala. Fomu hiyo amekabishiwa leo Juni 30,2025 na Katibu wa Umoja wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT)Wilaya ya Ilala ,Rosemary Mwakisalu Aidha,Senyange amesema kwamba ameamua kugombea Udiwani wa Viti Maalum ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea watanzania maendeleo

RAIS WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA RAJABU AMIRY AJITOSA UBUNGE JIMBO LA SEGEREA

Image
Na Mwandishi wetu ,DmNewsOnline              DAR ES SALAAM  RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Rajabu Amiry amesema amejitathimini na kuona ana sifa ndio  maana amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Jimbo la Segerea Kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Amiry amechukua fomu Juni 28,2025 na leo Juni 30,2025 amerejesha  na kukabidhi kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala ,Chief Sylvester Yeredi

MSAMA AJITOSA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA UKONGA

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsonline             DAR ES SALAAM  MFANYABIASHARA Maarufu jijini Dar es salaam na mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama leo Juni 29,2025  amechukua fomu ya kuomba ridhaa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga. Jimbo la ukonga lipo katika Halmashauri ya Manispaa Ilala ambapo pia ndio makazi ya Alex Msama . Msama amekabidhiwa fomu hiyo mapema leo  na Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala,ambaye pia Mkurugenzi wa Uchaguzi Wilayani humo Sylvester Yaredi.

KOKA ACHUKUA FOMU YA KUTETEA KITI CHA UBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJINI

Image
Na Mwandishi wetu,DmNews,Online,                    KIBAHA   ALIYEKUWA  Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Koka kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025  hatimaye  amejitosa kuchukua fomu kwa ajili ya kuendelea kutetea na kuwania  nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo  katika uchaguzi mkuu  ambao unatarajiwa kufanyika Mwezi Octoba mwaka huu lengo ikiwa ni kuendelea kushirikiana na wananchi katika kuwaletea chachu ya maendeleo. Koka akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo amesema kwamba nia na madhubumuni  yake makubwa ni kuhakikisha anaendelea  kushirikiana bega kwa bega na wananchi wa Jimbo la Kibaha mjini katika suala zima la kusikiliza changamoto walizonazo ikiwa pamoja na  kuwaletea maendeleo katika sekta mbali mbali. Koka amebainisha kwamba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ameweza kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo ikiwemo kufanikisha  kwa kiasi kikubwa kuweka ...

MLAWA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA KILOLO _IRINGA

Image
 Na Eliasa Ally DmNewsOline I                 RINGA  MDAU  wa maendeleo na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  wa Iringa, Aidan Mlawa, leo amechukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Kilolo kupitia chama hicho. Hatua hiyo inamuweka rasmi katika kinyang’anyiro cha kusaka ridhaa ya wananchi  kugombea ubunge kwa tiketi  ya chama hicho. Mlawa, amejijengea heshima kubwa kwa mchango wake katika shughuli za kijamii, amekuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi wa Wilaya ya Kilolo hususani wale walioko kwenye mazingira magumu, pamoja na kushiriki kwa karibu katika kupigania utekelezaji wa miradi ya maendeleo.   

MLAWA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA KILOLO _IRINGA

Image
 Na Eliasa Ally DmNewsOline I                 RINGA  MDAU  wa maendeleo na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  wa Iringa, Aidan Mlawa, leo amechukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Kilolo kupitia chama hicho. Hatua hiyo inamuweka rasmi katika kinyang’anyiro cha kusaka ridhaa ya wananchi  kugombea ubunge kwa tiketi  ya chama hicho. Mlawa, amejijengea heshima kubwa kwa mchango wake katika shughuli za kijamii, amekuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi wa Wilaya ya Kilolo hususani wale walioko kwenye mazingira magumu, pamoja na kushiriki kwa karibu katika kupigania utekelezaji wa miradi ya maendeleo.   

ACT WAZALENDO WAZINDUA OPERESHENI MAJI MAJI kWA NCHI NZIMA

Image
‎     Na  Mwandishi wetu,DmNewsOnline ‎               ‎DAR ES SALAAM  ‎ ‎CHAMA cha  ACT Wazalendo kimezindua rasmi operesheni Maji Maji itakayoanza kuanzia  Julai 1 hadi 15,2025 ambayo ni kampeni maalum ya kuwaamsha watanzania kurejesha thamani ya kura zao na kampeni hiyo itakuwa kwa nchi nzima na  itaongozwa na Kiongozi wa Chama Dorothy Semu. ‎ ‎Hayo yamebainishwa leo Juni 29,2025 Jijini Dar es Salaam na Naibu Mwenezi ,Shangwe Ayo  wakati wa mkuatano na waandishi wa habari  amesema kwamba baada ya kazi kubwa ya uimarishaji wa chama katika mgazi za majimbo na kuwapokea watu mbalimbali wanaojiunga na chama . ‎ ‎Naibu Mwenezi Ayo amesema kwamba ACT Wazalendo inafanya kazi ya kuunganisha makundi yote ya jamii  katika kulinda Demokrasia Yetu kwa kuhakikisha kuwa thamani ya kira inalindwa ifikapo Mwezi Oktoba 2025. ‎ ‎Aidha ,ameeleza kwamba katika Operesheni hiyo kutakuwa na misafara miwili ambapo msafara WA...

ALIYEKUWA MBUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA SAME MASHARIKI AJIUNGA NA ACT WAZALENDO

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline               DAR ES SALAAM  ALIYEKUWA Mbunge wa Viti Maalum  Same Mashariki (2020/2025) kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Nagy Livingstone Kaboyoka amejiunga na Chama cha ACT Wazalendo Leo Juni 28,2025 katika Ofisi za Makao Makuu ya  Chama hicho  Magomeni  Jijini Dar es Salaam  Kaboyoka  amepokelewa na Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo Dorothy Semu pamoja na viongozi wa ngome ya wanawake na viongozi wengine wa Chama katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema Makao Makuu ya Chama hicho. Aidha ,amesema ameamua kujiunga ACT Wazalendo kwa kuwa ni chama kinachopendwa na wengi kutokana na yale  wanayoyasimamia kwa maslahi kwa wote. Pia amesisistiza amani na haki na vifanyike katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na wao "iwe jua iwe mvua tutakaa kupigania haki yetu Hadi kieleweke",amesema Kaboyoka amewahi kuwa Mbunge wa kuchaguliwa Jimbo la Same Masha...

KASESELA ACHUKUA FOMU JIMBO LA RUNGWE.

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                      MBEYA  MJUMBE  wa NEC amechukua fomu kuwania ubunge jimbo la Rungwe lililopo Jijini Mbeya,Jimbo hilo ambalo linaongozwa na Mbunge Anton Mwantona hadi sasa. Mbali na kasesela pia  Jimbo hilo pia linanyemelewa na Gwamaka Mwafwenga aliyekuwa mkurugenzi wa NEMC,  yupo pia Eliud Mwaiteleke, Aliko Mwaiteleke na wengine ambao wameonesha nia ya Ubunge. Ikumbukwe kuwa Kasesela ameshashika nafasi mbalimbali ndani ya Chama na nje ambapo kwa upande wa Serikali ameshawahi kuwa mkuu wa wilaya ya iringa mjini.

KULWA BITEKO ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO JIPYA LA KATORO_GEITA

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                 KATORO _GEITA                 MUAMBATA  wa Balozi wa Tanzania nchini Uganda anayeshughulikia masuala ya fedha, Kulwa Masunga Biteko, amejiunga rasmi kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge kwa kuchukua fomu ya kugombea Jimbo Jipya la Katoro, lililopo Wilaya ya Geita, Mkoa wa Geita kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Biteko aliwahi kujitosa katika kinyang’anyiro cha ubunge mwaka 2020 kupitia chama hicho hicho, ambapo alipata kura 665 na kushika nafasi ya pili. Hatua yake ya sasa ya kuchukua fomu inaonyesha dhamira yake ya kuendelea kuwatumikia wananchi wa Katoro kupitia nafasi ya uongozi wa kisiasa ndani ya CCM. Jimbo jipya la Katoro limeonekana kuwa la moto baada ya makada mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi CCM kujitokeza kwa wingi kutaka ridhaa ya wananchi kwa kutinga bungeni mwaka ujao.