MSAMA AJITOSA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA UKONGA
Na Mwandishi Wetu,DmNewsonline
DAR ES SALAAM
MFANYABIASHARA Maarufu jijini Dar es salaam na mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama leo Juni 29,2025 amechukua fomu ya kuomba ridhaa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga.
Jimbo la ukonga lipo katika Halmashauri ya Manispaa Ilala ambapo pia ndio makazi ya Alex Msama .
Msama amekabidhiwa fomu hiyo mapema leo na Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala,ambaye pia Mkurugenzi wa Uchaguzi Wilayani humo Sylvester Yaredi.




Comments
Post a Comment