ALIYEKUWA MBUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA SAME MASHARIKI AJIUNGA NA ACT WAZALENDO
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA Mbunge wa Viti Maalum Same Mashariki (2020/2025) kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Nagy Livingstone Kaboyoka amejiunga na Chama cha ACT Wazalendo Leo Juni 28,2025 katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho Magomeni Jijini Dar es Salaam
Kaboyoka amepokelewa na Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo Dorothy Semu pamoja na viongozi wa ngome ya wanawake na viongozi wengine wa Chama katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema Makao Makuu ya Chama hicho.
Aidha ,amesema ameamua kujiunga ACT Wazalendo kwa kuwa ni chama kinachopendwa na wengi kutokana na yale wanayoyasimamia kwa maslahi kwa wote.
Pia amesisistiza amani na haki na vifanyike katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na wao "iwe jua iwe mvua tutakaa kupigania haki yetu Hadi kieleweke",amesema
Kaboyoka amewahi kuwa Mbunge wa kuchaguliwa Jimbo la Same Mashariki kupitia CHADEMA (2015-2020 na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC kwa miaka 10(2015-2025) ila alibwangwa na Anne Kilango Malecela wa CCM 








Comments
Post a Comment