KULWA BITEKO ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO JIPYA LA KATORO_GEITA

Na Mwandishi wetu,DmNewsonline

                KATORO _GEITA

               
MUAMBATA  wa Balozi wa Tanzania nchini Uganda anayeshughulikia masuala ya fedha, Kulwa Masunga Biteko, amejiunga rasmi kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge kwa kuchukua fomu ya kugombea Jimbo Jipya la Katoro, lililopo Wilaya ya Geita, Mkoa wa Geita kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Biteko aliwahi kujitosa katika kinyang’anyiro cha ubunge mwaka 2020 kupitia chama hicho hicho, ambapo alipata kura 665 na kushika nafasi ya pili.

Hatua yake ya sasa ya kuchukua fomu inaonyesha dhamira yake ya kuendelea kuwatumikia wananchi wa Katoro kupitia nafasi ya uongozi wa kisiasa ndani ya CCM.

Jimbo jipya la Katoro limeonekana kuwa la moto baada ya makada mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi CCM kujitokeza kwa wingi kutaka ridhaa ya wananchi kwa kutinga bungeni mwaka ujao. 


Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.