ACT WAZALENDO WAZINDUA OPERESHENI MAJI MAJI kWA NCHI NZIMA
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
CHAMA cha ACT Wazalendo kimezindua rasmi operesheni Maji Maji itakayoanza kuanzia Julai 1 hadi 15,2025 ambayo ni kampeni maalum ya kuwaamsha watanzania kurejesha thamani ya kura zao na kampeni hiyo itakuwa kwa nchi nzima na itaongozwa na Kiongozi wa Chama Dorothy Semu.
Hayo yamebainishwa leo Juni 29,2025 Jijini Dar es Salaam na Naibu Mwenezi ,Shangwe Ayo wakati wa mkuatano na waandishi wa habari amesema kwamba baada ya kazi kubwa ya uimarishaji wa chama katika mgazi za majimbo na kuwapokea watu mbalimbali wanaojiunga na chama .
Naibu Mwenezi Ayo amesema kwamba ACT Wazalendo inafanya kazi ya kuunganisha makundi yote ya jamii katika kulinda Demokrasia Yetu kwa kuhakikisha kuwa thamani ya kira inalindwa ifikapo Mwezi Oktoba 2025.
Aidha ,ameeleza kwamba katika Operesheni hiyo kutakuwa na misafara miwili ambapo msafara WA kwanza utaongozwa na Kiongozi wa Chama na msafara mwingine utaongozwa na Kiongozi mstaafu Zitto Kabwe.
Pia amesema kwamba Kiongozi wa Chama ataongozana na Makamu Mwenyekiti Bara,Isihaka Mchinjita na watakwenda majimbo yaliyopo kwenye Mikoa ya Kigoma,Simiyu,Shinyanga,Arusha,Kilimanjaro,Tanga na Dar es Salaam.
Sambamba na hayo msafara wa Kiongozi wa Chama Msataafu, Zitto Kabwe pamoja n Naibu Katibu Mkuu Bara Ester Thomas watakwenda kwenye majimbo yaliyopo kwenye mikoa ya Tabora,Katavi,Rukwa,Mbeya,Ruvuma,Selous,Mtwara,Lindi na Mwambao.
Amemalizia kwakusema kwamba ziara hii pia itaambatana na mikutano ya hadhara,viongozi watafanya vikao vya ndani vitakavyojumuisha wajumbe wa Mikutano Mikuu pamoja na watia Nia wa Ubunge na Udiwani




Comments
Post a Comment