POLISI DAR WATOA RAI KWA WATUMIAJI VYOMBO VYA MOTO KUFUATA SHERIA
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa rai kwa watumiaji wote wa barabara kuzingatia Sheria, Kanuni, na matumizi sahihi ya barabara muda wote wanapoendesha vyombo vya moto.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 31,2025 Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalu ya Dar es Salaam,SACP Muliro Jumanne Muliro amesema mwezi Aprili hadi 31 Mei 2025 jumla ya madereva wa magari na pikipiki za maguruduamu matatu (Bajaj) wamekamatwa kwa kutumia barabara za mwendo kasi kinyume na sheria ni 289, pikipiki(bodaboda) 61, bajaj 65,magari ya Serikali 35, magari binafsi 123,walichukuliwa hatua kali za kisheria na wengine 41walionywa.
Aidha ,amesema kwa kutumia kifungu Cha 45 na 46A vya Sheria ya Usalama barabarani sura ya 168 iliyorekebishwa mwaka 2002 kinachokataza dereva kutumia kilevi na kuendesha chombo Cha moto,ufuatiliaji maali usiku na mchana ulifanywa na kuwapima ulevi madereva kwadharura.
Hata hivyo jumla ya madereva 19 walikamatwa wakiwa walevi kwa kuzidisha kiwango cha kisheria ambacho ni 0.8mls ambapo Mkoa wa Kinondoni walikuwa 18 na Ilala alikua mmoja.
Vilevile madereva wa
magari ya abiria walikuwa 3 ambao kwa mujibu wa kanuni zinazosimamia
sura 168 iliyorekebishwa mwaka 2002 kifungu cha 49 inaelekeza kuwa
usafiri wa umma yaani Land Transport Legulations Authority Act sura ya 413 ya mwaka 2020, G.N no.81 kifungu cha 10 (1) (b)hairuhusiwi
kwa dereva kutumia kiwango chochote
cha ulevi na kuendesha gari la
abiria.
Madereva 14 wamefikishwa mahakamani, madereva 3 wamefungiwa leseni na madereva 2 waliandikiwa faini.
Sanjari na hayo ,Januari 2023 hadi Mei 2025 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ilipeleleza na kuwakamata watuhumiwa mbalimbali ambao baadhi yao walifikishwa kwenye mahakama tofauti zilizopo jijini kwa tuhuma mbalimbali za kesi za ulawiti,ubakaji unyanganyi wakutumia silaha mashauri yao yalifikishwa mahakamani na kupatikana na hatia za vifungo vya maisha jera ,kufungwa miaka 60 jera pamoja na kufungwa miaka 30 jera.
Comments
Post a Comment