WANANCHi WAMETAKIWA KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA
Na Mwandishi wetu,DmMewsOnline
DAR ES SALAAM
MHIFADHI Historia Makumbusho ya Taifa, Shomari Rajabu Shomari amewata wananchi kutembelea makumbusho ya Taifa kwani ni sehemu sahihi ya kujifunza na kujione historiambalimbali.
Hayo ameyabainisha leo Aprili 25,2025 Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara maalum ya Maafisa Utamaduni na Maafisa Maendeleo ya Michezo.
"Makumbusho ni sehemu ambayo wanapokea wageni mbalimbali na taasisi ambapo Leo tumepokea maafisa utamaduni toka mikoa tofauti tofauti wamekuja kujifunza jinsi makumbusho yanavyohifadhi historia yeti pamoja na utamaduni",amesema
Aidha ,amesema kwamba mwamko wa watu kuja kujifunza kwani huwa tunaandaa programu mbalimbali kwa ajili ya kujifunza.
Pia amewakaribisha watanzania kutembelea makumbusho hasa siku ya tarehe 26,Aprili 2025 kwa lengo la kujifunza na na kuelimika zaidi jinsi waasisi wetu waliopigania Muungano wetu na kuona ule mchanga uliotumika kuchanganywa kati ya Tanganyika na Zanzibar.
Pia Mhifadhi Shomari Kuna vitu vingi vinavutia watalii,fuvu la mwanadamu wa kwanza ,zipo kumbi mbalimbali zilizibeba historia pamoja na fedha za zamani fedha za kilwa pamoja na inajihusisha na kufanya tafiti mbalimbali.
Naye Afisa Michezo Mkuu OR TAMISEMi George Mbijima amesema wao kama wasimamizi na watekelezaji wa sera zinazohusiana masualana uhifadhi utamaduni tunao maafisa ambapo mambo haya yanapoibuliwa hivyo wameanzisha vitengo maalum .
Aidha ametoa wito kwa maafisa kuanzia Vijiji,Kata,Tarafa ,Halmashauri na Mikoa kubaini,kutambua na kuweka mikakati ya kuhifadhi utamaduni huu ili kuja kurithisha vizazi vijavyo kwani ili jamii iwe imaralazima kujua historia yake tangu ilipotoka hadi ilipofikia.
Kwa upande wake Afisa Utamaduni Nachigwea Lindi ,Muhsini M.Izza amesema kwamba kutembelea makumbusho tumejifunza mambo mengi ambayo yalikuwepo katika Taifa letu hapo awali yametunzwa katika eneo hili ili sisi kupata kutambua wenzetu walianzia wapi na kutokea wapi ili sisi Maafisa tuweze kutunza na kuendelezana kuibua mambo mbalimbali kwa ajili ya kuweka alama katika Taifa
Comments
Post a Comment