TLP KINAWATA WANACHAMA WENYE SIFA KUJITOKEZA KWA WINGI KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
. DAR ES SALAAM
CHAMA cha Tanzania Labour Party(TLP) kinapenda kuwataarifu na kuwatangazia wanachama wote pamoja na wananchi na wapiga kura kuwa kimeanza kutoa fomu za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Ubunge na Udiwani kuanzia Aprili 25,2025.
Akizungumza na mwandishi wa habari wa DmNewsOnline kwa mahojiano maalum Ofisi kwake leo Aprili 30,2025 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa TLP Taifa,Richard Lyimo amesema kwamba fomu za Urais zinapatikana Makao Makuu ya Chama Dar es Salaam na Ofisi ndogo za Zanzibar na zoezi la kuchukua fomu lilianza Aprili 25,2025 na mwisho ni Mei 15,2025 kwa wagombea wa Urais.
Aidha,Mwenyekiti Lyimo amesema kuwa fomu za Ubunge na Udiwani zinapatikana kwenye ofisi zetu za Mikoa,Wilaya na Majimbo kwa nchi nzima kwa wenyeviti wa Mikoa,Wilaya,Majimbo na Makatibu na zimeanza kutolewa Aprili 30,2025 hadi Juni 20,2025.
Mwenyekiti Lyimo amesisitiza wanachama kuzingatia muda wa kurejesha kwa ajili ya kupitishwa kwenye vikao maalum vya kupitisha wagombea.
Pia amewataka wanachama kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo kwani hiyo ni fursa muhimu kwa chama.
Hata hivyo ,Mwenyekiti Lyimo amewata vijana na wanawake wenye sifa za kuwania nafasi za udiwani na Ubunge kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu.
"Wengi wajitokeze kwenye chama chetu kwani tunahitajo wabunge na madiwani wakutosha na dhamira ya chama ni kusimamisha wagombea nchi nzima na amewata wananchi kujiunga naTLP",alisema Mwenyekiti Lyimo
Sambamba na hayo amesema mkutano maalum wa kuchagua Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar utatangazwa hivi karibuni.
Vilevile Mwenyekiti Lyimo amesema kwamba anatia nia ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Bunjo Mkoa wa Kilimanjaro.
Ameahidi kwa wananchi wa Jimbo Hilo kwamba mwaka huu ni wakuweka historia kwa kuchagua watu wenye uchungu na jimbohilo sio watu wenye uchu wa madaraka.
"Ng'ombe hachaguliwi kwasababu ya kuangalia mapembe,ng'ombe anaangaliwa namna alivyonona lakini ukiangalia mapembe unaweza kuona ng'ombe lina mapembe makubwa lakini halina faida,Mimi nataka kwenda kufanya kazi ya wananchi",alisema Lyimo


Comments
Post a Comment