MWENYEKITI MLALE KINYAMWEZI ATANGAZA NEEMA YA MIKOPO KWA WANANCHI WAKE.

Na Mwandishi wetu,DmNewsonline 

               DAR ES SALAAM 

UONGOZI wa Serikali ya Mtaa wa kinyamwezi uliopo kata ya Pugu Wilayani ilala  chini ya Mwenyekiti wake Fahad Mlale(Bilionea) umetangaza Neema ya kuwapatia mikopo wananchi wake na hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa .

Akizungumza katika mkutano wa Kwanza wa wananchi tangu kuchaguliwa kuwa kiongozi wa mtaa huo Mwenyekiti Mlale kwaza aliweza kuwashukuru wananchi hao kwa kuweza kumwamini na kuchagua kuwa kiongozi wao na pili amewaeleza wananchi hao kuwa kazi iliyopo mbele Yao ni kuujenga mtaa huo.

Mkutano huo ambao umefanyika Machi 25 ,2025 katika ofisi za Serikali hiyo mtaa mwenyekiti pamoja na mambo mengine amewaeleza wananchi wake kuwa wakati akijinadi ili kupata ridhaa ya kuwa mwenyekiti alihaidi wakimchagua basi atahakikisha anatoa mikopo kwa makundi mbalimbali hivyo basi kuazia mei 18 mwaka huu ataaza kutoa mikopo hiyo.

"Hiii ni ahadi yangu kwenye .natangaza rasmi kwamba kuazia mei 18 mwaka huu tutaaza kutoa mikopo midogo kidogo kwa wananchi na tumeshatenga milioni 20 kwa ajili ya jambo hili .kitu kikubwa ni uaminifu na riba yake itakuwa rafiki ambayo haifanani na mikopo inayoumiza kama Ile ya maisha damu ."amesema Mlale

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amezungumzia kuimarisha ulinzi shirikishi ambapo amesema atahakikisha ananunua vifaa vya kisasa vitakavyorahisisha utendaji kazi kuwa rahisi ukilinganisha na ilivyo sasa.

Amesema ataninua rediocall ,tochi kubwa za kuangaza kwa umbali zaidi, malungu ya kisasa ,butu pamoja na vifaa vingine ili kurahisisha shughuli hizo za ulinzi kwa urahisi zaidi.

Mambo mengine yaliyozungumza katika mkutano huo ambapo wananchi wameweza kutoa kero zao ni pamoja na huduma za maji kwamba maji kutoka kwake imekuwa changamoto lakini wanakuwa wepesi kutoa taarifa za bili na wakati mwingine meseji za bili zinakuja hata mwezi ukiwa bado haujamalizika.

Pia wananchi katika mkutano huo wameueleza uongozi huo wa Serikali za mitaa kuhakikisha wanatafuta namna ya kujenga uzio katika shule ya sekondari kinyamwezi kwani shule hiyo Iko wazi jambo ambalo ni hatari kwa wanafunzi hususani watoto wakike.

Malalamiko mengine kutoka kwa wananchi ili kuwa nikuchangishwa fedha Kwa wanafunzi wa shule ya msingi mtaani humo ambapo zinadaiwa kuwa ni fedha kwa ajili ya mitihani ya majaribio  na endapo mwanafunzi anakuwa hana fedha hiyo basi ananyang'anywa hadi pesa yake ya kula ambayo anapewa na mzazi.

Kutoka na changamoto hizo ambazo ziliibuliwa na wananchi kupitia mkutano huo wa kikanuni wa Serikali ya Mtaa mwenyekiti amewaeleza wananchi hao kuwa kero zote amezichukua na anakwenda kuzipeleka mahala husika na nyingine watazitafutia ufumbuzi kwa maslahi ya maendeleo ya Mtaa huo.

Katika mkutano huo viongozi mbalimbali hudhulia wakiwemo watalamu kutoka Dawasa, lakini Polisi kata  naye alikuwepo pamoja na wenyeviti wengine waalikwa kutoka mitaa mingine ambao nao walipata wasaa kutoa michango Yao huku wananchi wakiomba kutoa  ushirikiano kwa mwenyekiti huyo kwasababu ni mpya kwenye siasa na uongozi.




Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025