MABONDIA WAPIMANA UWEZO KUELEKEA. KNOCK OUT YA MAMA MEI 24,2025.
Na Mwandishi wetuDmNewsOnline
DAR ES SALAAM
MSIMU wa nne wa Knock Out ya Mama unatarajiwa kufanyika Mei 24,2025 Jijini Dar es Salaam ,hivyo mabondia mbalimbali wamekuta kupimana uwezo kwa kufanya mazoezi kwa lengo la kujifunza na kujiimarisha pambano hilo lililopewa jina sparring lilihusisha mabondia mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Pambano hilo la Sparring limefanyika Aprili 26,2025 lilofanyika katika gym ya Mbezi Msumi ya Kampuni ya Mafia Boxing eneo la msitu wa Mwabepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo mabondia walipanda ulingo kwa kupima .
Akizungumza wakati wa zoezi hilo la sparring Kocha wa Gym ya Mafia Boxing Hamfrey Mohamed Said alisema kuwa hatua hii ni sehemu ya maandalizi kuelekea awamu ya nne ya mchezo wa Knocking Out ya Mama itakayochezwa hivi karibuni.
Kocha Said amesema sparring hii ni kwa ajili ya kujua kwamba yale mazoezi ambayo tumewafundisha mabondia wetu kama mazoezi yamewajengea uwezo .
"Kwa mazoezi haya mpaka sasa tumeona kwamba mabondia wako vizuri kwa asilimia 99 na baadhi ya mapungufu tutayafanyia kazi" alisema
hivyo tunawakaribisha mashabiki wote wa ngumi kuja kujionea pambano hili ",amesema
Kwa upande wake Bondia wa ngumi za kujitegemea wa kulipwa Tanzania,,Haidary Mchanjo amesema wanaushukuru uongozi wa Mafia Boxing kwa kuandaa mazoezi hayo ya sparring kwani yamewakuatanisha na mabondi wakubwa kwa ajili ya kubadilishaba uzoefu
Aidha,amejiandaa vizuri kwa pambano hilo lijalo na amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa kwa kuwapa motisha kwenye mchezo wa ngumi kwani ngumi zimetambulika kama kazi nyingine ametutia nguvu na kutambua vipaji vya mabondia.
Pia Mchanjo ameelez kwamba zamani mchezo wa ngumi ulionekana kama ni mchezo wa wahuni lakini sasa ni mchezo unaotambuliki na unatuingizia kipato.
Naye Mchanja Yohana aka( Kompyuta master) bondia wa Mafia boxing amesema
sparring imenipa maandalizi mazuri kuelekea mchezo kwani tumejipima utimamu wa mwili tunaamini awamu ya nne ya Knock out ya Mama tumejipanga ipasavyo kuingia ulingoni.
(Naishukuru Kampuni ya Mafia Boxing kwa kuamua kutuweka pamoja mabondia kupitia mazoezi haya ya sparring kwa hiyo naahidi kufanya vizuri kwa kumchapa mpinzani wangu katika knock out ya awamu ya nne itakayochezwa hivi karibuni
Comments
Post a Comment