MATUMLA AMEWATA WATANZANIA KUJITOEZA KWA WINGI KWENYE PAMBANO LA FEBRUARI 28,MWAKA HUU.
Na Mwandishi wetu ,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
BONDIA Amiri Matumla amewaomba watanzania kujitokezq kwa wingi kushuhudia pambano litakalofanya Februari 28,2025 dhidi ya mpimzani wa kutoka Namibia ,Paul Amavila katika Ukumbi wa Magomeni Sokoni Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari Februari 25, 2025 Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion, 'Knock Out ya Mama' Ally Zayumba na kufafanua kwamba bondia huyo katika pambano hilo atazichapa na mpinzani wake kwa mizunguko nane.
Zayumba amesema kwamba hili ni pambano lake la kwanza tangu ajiunge kwenye mapambano ya ngumi za kulipwa na ameahidi kufanya vizuri kwa lengo la kuanza kuweka rekodi nzuri katika karia yake kupitia masumbwi.
Aidha, amesema katika pambano hilo kutakuwa na mapambano mengine 11 ya utangulizi yakiongozwa na mkongwe Dullah Mbabe.
Ameeleza kuwa huu ni msimu tatu kwa mapambano ya aina hiyo kufanyika chini ya Mafia Boxing Promotion yakiwa na lengo la kunadi miradi iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha amefafanua kwamba Michezo yaa ngumi katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Dkt Samia, umekuwa na mafanikio makubwa hivyo ni vema watanzania wakaendelea kumuunga mkono.
Amefafanua kwamba viingilio vitakuwa ni shilingi, 50,000, sh. 20000 na 10,000 na mabondia wote watapima uzito katika Ukumbi huo Feb 27,2025
Hata hivyo Zayumba amewataja mabondia wengine watakaopanda ulingoni katika mapambano hayo kuwa ni Oscar Richard atakayezipiga na bondia kutoka Malawi.
Rashid Mtange kutoka Nacoz Camp chini ya kocha Ramadhani Uhadi 'Rama Jah' atazichapa na bondia kutoka India na wengine.
Bondia Matumla ni mtoto wa Rashid Matumla' Snake Man' amejinasibu kufanya vizuri pambano hilo kwakuwa amejiandaa vizuri na kufanya maandalizi ya kutosha.
Comments
Post a Comment