TMA YATOA TAHADHARI MWENDELEZO WA MVUA ZA VULI NOVEMBA 2024 HADI APRILI ,2024


Na Angelina Mganga,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM 

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza muelekeo wa msimu wa mvua za vuli ambazo zimeanza Novemba 2024 na kuishia mwezi Aprili,2025.

Akizungumza na Waandishi wa habari  Oktoba 31 ,2024,Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka  Dkt.Ladislaus Chang'a amesema kutokana na mabadiliko ya hali ya mifumo ya hali ya mvua nchini inaonekana kupungua kupelekea mvua katika maneno mengi kuwa chini ya wastani.

Taarifa ya tahadhari imetolewa  kutokana na  mabadiliko ya hali ya hewa na mifumo mingi inaonyesha joto  kuongezeka Duniani  ukilinganisha na mwaka 2023, kwenye usawa wa Bahari maeneo mengi ya Kusini mwa Bahari ya Hindi.

Msimu wa Vuli kwa miezi ya Oktoba hadi Disemba, 2024 katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka  kwa Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia pamoja na Zanzibar (visiwa vya Unguja na Pemba utabiri wake ulitolewa tarehe 22 Agosti, 2024. Mvua za Chini ya Wastani hadi Wastani zilitarajiwa katika maeneo mengi ya Pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini Mashariki. Aidha,kwa maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria mvua zilitarajiwa kuwa za Wastani hadi Chini ya Wastani hivyo kupelekea vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko wa mvua usioridhisha.
 
 
Aidha, mvua hizo zilitarajiwa kuanza kwa kusuasua wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2024 katika ukanda wa Ziwa Victoria na kusambaa katika maeneo mengine yanayopata mvua za Vuli kati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi.

"Ushauri na tahadhari umetolewa kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za Hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama kilimo na usalama wa chakula,mifugo na uvuvi,maliasili,wanyamapori,na utalii,nishati na maji,usafirishaji(nchi kavu kwenye maji na angani),mamlaka za miji,afya,sekta binafsi pampja na menejimenti za maafa",amesema



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025