UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI
Na Mwandishi Wetu DAR ES SALAAM UONGOZI wa Shirikisho la Vyama vya Waganga wa Tiba Asili Tanzania (Shivyatiata) uliokasimishwa madaraka ya muda wa mwaka mmoja kuliongoza hadi likae sawa, unalalamikiwa na wachama wa vyama vya waganga wa tiba asili nchini kwa kuhodhi madaraka kwa miaka nane kinyume cha sheria na utaratibu waliokubaliana. Wakizungumza na Mwandishi wa DMNews online Tanzania Disemba 31, 2025 baadhi ya wanachama wa vyama vya waganga wa tiba asili kutoka vyama 28 vinavyounda shirikisho hilo, kwamba uongozi uliopo si halali wakidai haukuchaguliwa kikatiba. Pia, wamesema kuwa uongozi huo wa Shirikisho umeshindwa kutimiza majukumu na malengo ya Serikali kuukasimisha madaraka ya muda badala yake unalitumia kujinufaisha wenyewe ikiwamo kufifisha shirikisho kwa kulikosesha dira. Mwenyekiti wa Umoja wa Watengeneza Bidhaa Asili Tanzania (UWABIATA) Rajab Ha...

Comments
Post a Comment