CARITAS TABORA YATOA VYEREHANI VYA ZAIDI YA M.17 KUSAIDIA WANAWAKE VIJIJINI



Na Benny Kingson,DmNewsOnline
TABORA

 JUMLA ya vyerehani 54 vyenye thamani ya sh.milioni 17,820,000 vimetolewa na idara ya maendeleo ya jamii ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Tabora CARITAS  kwa wanawake ‘walea pweke’ wa Vijiji vya wilaya ya Uyui Mkoani humo kwa lengo la kuonyesha upendo kwao na kuwakwamua kuichumi.

Mkurugenzi wa CARITAS Mkoani Tabora Padri Paschal Kitambi akikabidhi vyerehani hivyo kwa wanawake hao ‘Single mother’ katika Kata ya Isikizya wialayani humo alisema kuwa lengo la msaada huo ni kuonyesha upendo wao  kwa vitendo  na kuwakwamua kimaisha.

Padri Kitambi amesema kuwa idara hiyo imewashika mkono akinamama hao ambapo nao wanatakiwa kuinuka na kuendeleza jitihada za kujipatia vipato,kujiimarisha kiuchumi na hatimaye kujiletea maendeleo yao na kuwa mfano bora kwa jamii.

‘CARITAS imewashika mkono na mkumbuke Kanisa linasisitiza upendo kupitia salamu ama kauli mbiu yetu ya dini mbalimbali,upendo na amani,hivyo na nyie msimame msonge mbele na kuonyesha upendo huo kwa wengine kwa kufanya maendeleo makubwa zaidi ya haya’amesema.

Makamu Mwenyekiti wa kikundi cha tunda jema Mwajuma Jumanne akisoma risala yao alisema kuwa wana vikundi 10 vilivyo jumla ya wanachama 124 waliopatiwa mafunzo ya ujasiriamali na masuala ya kuweka na kukopo SACCOS ambapo wamfanikiwa kupata uelewa wa kutosha.

Amesema CARITAS ILIWAWEZESHA SH.500,000 kila kikundi ambapo wameweza kukopeshana na kufanya shughuli mbalimbali za kuwaingizia viapato vya kuendesha maisha yao na waliiomba idara hiyo kupanua wigo wa mafunzo wanayowapa kwa kuwapeka nje ya wilaya hiyo kwwenda kujifunza na kubadilisha ujuzi na watu wa maeneo mengine.

Hawa John (26) mkazi wa Kata ya Ilolwansimba na  Sada Maasudi (28) wa Kata ya Isikizya walisema kuwa vyerehani hivyo walivyopewa na CARITAS vitawasaidia kuwapatia vipato vyao na kwamba idara hiyo imewawezesha kujiunga katika vikundi na kupta elimu ya VICOBA vinavyowasaidia kukopeshana na kuinua hali ya uchumi wa familia zao.

Mratibu wa mradi huo wa kuwawezesha wana wake hao Haruna Nelson alisema kuwa CARITAS imetoa vyerehani hivyo ambapo kila kimoja kinathamani ya sh.330,000 na kwamba wamewapa mafyunzo ya kuwajengea uwezo na kuwapatia watoto wao sare za shule.

Nelson amesema kuwa idara yao ikiwa chini ya Kanisa hilo inasisitiza suala la upendo katika jamii na kusaidiana bila kujali ama kubagua kwa itikadi ya dini,kabila au muonekana wa mtu na kwamba imewasaidia wana wake hao ambao wapo walioachwa na wenzi wao kwa kutelekezwa na kufariki dunia.

Amewahimiza wanawake wengine wajiunge katika vikundi vitavyoratibiwa na CARITAS ambapo watapatiwa mafunzo na kuwezeshwa na watajihakikishia maendeleo ya uhakika na kuwa na maisha bora wao pamoja na familia zao na taifa kwa ujumla na kwamba kazi itaendelea daima.



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025