DIWANI VISIGA AMUUNGA MKONO RAIS DKT. SAMIA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU



Na Victor Masangu,DmNewsOnline
KIBAHA 
 
DIWANI wa kata ya Visiga katika Halmashauri ya mji Kibaha Kambi Legeza katika kuunga mkono na  kuchagiza  chachu ya maendeleo katika sekta ya elimu ameamua kutoa msaada wa mtambo  maalumu wa kusaidia  kutolea nakala mbali mbali za karatasi  'Photocopy mashine'  katika shule ya msingi visiga kwa ajili ya kuwasaidia walimu na wanafunzi kuondokana na adha waliyokuwa nayo.

 Kambi ametoa msaada wa mashine hiyo wakati  wa sherehe ya  mahafali ya shule ya msingi Visiga ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuweza kuwaaga wanafunzi wanaomaliza  darasa la saba wapatao 248 ambao wamefanikiwa kuhitimu katika hatua hiyo ngazi ya msingi  na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali, wakiwemo wa  chama, wazazi , walimu,  walezi pamoja  na wazazi.

Kambi amesema  kwamba amesema kwamba ameamua kutoa msaada huo kutokana na  kubaini katika shule hiyo kuna uhitaji mkumbwa kupeleka mashine hiyo ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa katika kuwasaidia walimu na wanafunzi ambao wamekuwa wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo kutumia gharama kubwa hivyo itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa upande wao.

"Mimi kama Diwani wa kata ya Visiga nimebaini kuna changamoto kubwa na wazazi na walezi kuchanga michango mbali mbali kwa ajili ya kutoa nakala za mitihani hivyo kunatumika gharama nyingi sana kwa hivyo nikaona kuna umuhimu mkubwa kupitia mahafali haya niweze kutoa mashine hii ya Photocopy ambayo  nina amini itaweza kuleta mageuzi makubwa katika shule hii ya msingi Visiga,"amesema Kambi  

Pia ameongeza kwamba lengo lake kubwa ni kuweza kuweka mikakati kabambe kwa ajili ya kumsaidia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo hivyo ameahidi kuendelea kutoa sapoti katika shule nyingine zilizobaki ili kuweza kukuza na kuboresha sekta ya elimu kwa ngazi ya msingi na Sekondari  katika Kata ya Visiga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya  shule ya Visiga Kasmir Komba amempongeza kwa dhati Diwani huyo kwa kuweza kutoa mashine hiyo ambayo itaweza kwenda kupunguza changamoto ya siku nyingi ambayo ilikuwa inawakabili katika suala zima la kutoa nakala mbali mbali hasa katika kipindi cha kutolea mitihani na mambo mengine ya muhimu.

Mwenyekiti huyo ameongeza kwamba shule hiyo ambayo imeaanzishwa  mnamo  mwaka 1992 imekuwa ikifanya vizuri  kwa wanafunzi wake katika mitihani mbali mbali  japo inakabiliwa na baadhi ya changamoto mbali mbali zikiwemo uhaba wa madawati, pamoja na uchakavu wa madirisha kwa baadhi ya madarasa.

Nao baadhi ya wazazi ambo wamehudhuria katika mahafali hayo akiwemo Zainabu Abdalah hawakusita kutoa pongezi zai za dhati kwa Diwani wa kata ya Visiga ambaye ameweza kuondoa kero ya michango mbali mbali ambayo walikuwa wakichangishwa na walimu kwa ajili ya kutoa nakala za mitihani hivyo mashine hiyo itawaondolea kabisa baadhi ya michango.

Amefafanua kwamba kabla ya kutolewa kwa mashine hiyo hapo awali wazazi na walezi walikuwa wanachangia kiais cha shilingi elfu 1200 ili mtoto aweze kupata huduma ya kufanya mitihani jambo amabalo lilikuwa ni usumbufu mkubwa kutokana na hali ya kipato na uchumi waliyonayo lakini kwa kitendo alichokifanya diwani huyo kinafaa kuigwa kwa viongozi wengine.



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025