WHI NA MKANDARASI SHADONG HI-SPEE GROUP WATIA SAINI MKATABA UJENZI WA NYUMBA 101.
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
MKURUGENZI Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI) Dkt.Fred Msemwa amesaini mkataba wa ujenzi wa nyumba 101 zitakazojengwa eneo la Mikocheni Regent Estate Jijini Dar es Salaam.
Mkataba huo ni baina ya WHI na Mkandarasi Shadong Hi-Speed Group ambapo utiaji Saini umefanyika leo Julai 30,2024 katika Ofisi za WHI jijini Dar es salaam
Dkt.Msemwa amesema ujenzi huo utaanza mwezi Agosti 2024 na unahusu ujenzi wa jengo la ghorofa 12 lenye nyumba 101 ambapo Kila mnunuzi atamilikishwa nyumba atakayonunua ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma.
Aidha amesema WHI tayari imejenga nyumba 1,003 katika mikoa 19 nchini Tanzania na sehemu ya nyumba 218 zitajengwa katika mikoa ya Dodoma,Lindi,Mtwara,Singida,Pwani na Ruvuma katika mwaka wa fedha 2024/2025.
"Ujenzi wa mradi huu wa nyumba 101 utagharimu kiasi Cha shilingi Bilioni 18.6 na ujenzi wake utafanyika kwa kipindi cha miezi 18.Nyumba hizi zitauzwa kwa utaratibu maalum wa unafuu kwa watumishi wa umma",amesema Mkurugenzi Mtendaji Dkt.Msemwa.
Mkurugenzi Mtendaji Dkt.Msemwa ameeleza kwamba Bei ya nyumba ya chumba kimoja yenye sebule,chumba Cha kulala,choo,stoo,jiko,balcony itaanzia shilingi Milioni 99 na Bei ya nyumba ya vyumba vitatu vya kulala,sebule,stoo,balcony itaanzia shilingi milioni 234/=.
"Bei ya nyumba hizi zikilinganisha na nyumba za aina hii katika eneo la Mikocheni,nyumba hizi ni nafuu Kwa kati ya asilimia 10% Hadi 40%.Uuzaji wa nyumba hizo tayari umeanza,na tunatarajia mwitikio mkubwa kutoka kwa walengwa.Huu ni mradi unaolenga kuwapa watumishi wa umma guess Bora za umiliki wa makazi yenye thamani na ubora",alisema Dkt.Msemwa.
Watumishi Housing Investment ni taasisi ya umma chini ya Ofisi ya Rais UTUMISHI yenye jukumu la uendelezaji wa milki na usimamizi wa uwekaji kupitia uanzishaji na usimamizi wa mifuko ya uwekezaji wa Pamoja.WHI inasimiw mifuko miwili yaani Mfuko wa Nyumba Pamoja na mfuko wa Faida Fund.
Comments
Post a Comment