RAIS SAMIA ARIDHIA KINANA KUJIUZULU CCM



Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline 

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amejiuzulu wadhifa huo baada ya Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuridhia ombi lake.

Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa leo Julai 29, 2024 na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makala akisema Kinana ameandika barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM Samia amesema "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako." Imesema taarifa hiyo.

Pia Samia amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Kinana kila itakapohitajika. 

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025