WASHINDI WAWILI WA SHINDANO LA UUZAJI NA USAMBAZAJI VILAINISHI VYA ORYX KWENDA DUBAI




Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
 DAR ES SALAAM

KAMPUNI  ya Oryx Services and Specialties ltd  imeendesha shindano la wauzaji na wasambazaji wa vilainishi vya Oryx  Energies na kupata washindi wawili  ambao wamejishindia safari ya kwenda Dubai na Leo Mei 31 ,2024 wameweza kukabidhiwa tiketi zao.

Hafla hiyo fupi ya makabidhiano tiketi imefanywa na Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Kalpesh Mehta kwenye ofisi za Kampuni hiyo zilizopo Kinondoni _victoria ambapo pamoja na mambo mengine  amesema Kampuni ya Oryx Services and Specialties Ltd iliendesha shindano hilo la wauzaji (Mawakala)na wasambazaji  kati ya Maduka ya Oryx na wasambazaji wa Vilainishi vya Oryx. 

Mehta amesema shindano hilo lilianza Januari na kumalizika Desemba 2023 na kwamba leo hii wametangaza washindi wa shindano hilo ambao ni Mbise Oil Shop iliyopo Arusha (Oryx Shop) na Lwimba Investment Company Ltd iliyopo Dar es salaam (Msambazaji).

Ameongeza kuwa zawadi wa shindano hilo amepata Safari ya kwenda Dubai ambapo leo washindi  wamekabidhiwa tiketi zao tayari kwa safari huku akifafanua gharama zote za safari hiyo ya siku nne  Dubai zimelipiwa na kampuni ya Oryx Services and Specialities Limited. Kila mshindi amepata tiketi mbili kwa ajili ya safari ya Dubai.

"Tunatarajia kutangaza mashindano yafuatayo hivi karibuni ambayo yatakuwa ya kusisimua zaidi kuliko shindano lililopita.Ni matumaini yetu wauzaji wetu wote watashiriki tena vyema kama mwaka uliopita.

"Oryx Energies ni kampuni kubwa na ya muda mrefu ya kimataifa inayotoa huduma za nishati barani Afrika. Oryx Energies huagiza, kuchakata, huhifadhi na kusambaza bidhaa za mafuta ya magari, machine na mitambo (Dizeli, Petroli, Vilainishi) na gesi za kupikia (LPG) zitumikazo katika sekta mbalimbali za uchumi.

 "Ni msambazaji namba moja wa bidhaa za mafuta na vilainishi katika sekta ya uchimbaji madini (migodi). Pia Oryx Energies inaongoza kusambaza vilainishi katika sekta zingine za kiuchumi kama usafirishaji wa nchi kavu (pikipiki, magari, treni) na majini, viwandani, ujenzi na kilimo.

Pia  Oryx Energies huzalisha na kusambaza vilainishi mbalimbali kuanzia vya magari, mitambo ya migodini na viwandani, uzalishaji wa umeme nk ambavyo vimeidhinishwa na Watengenezaji wakubwa wa Vifaa Halisi (Original Equipment Manufacturers) na vinakidhi au kuzidi viwango vya kimataifa. 

Ameongeza katika kuhakikisha bidhaa na huduma zinapatikana kwa watumiaji kote nchini, Oryx Energies inaendelea kuboresha njia zake za usambazaji kwa kupitia Maduka ya Kipekee ya Kampuni (CODOs), Wasambazaji na vituo vya mafuta vya Oryx.
 
Akizungumza kwa niaba ya washindi , Vaileth Cilwimba kutoka Lwimba Investment Company Ltd jijini  Dar es salaam (Msambazaji) amesema ushindani ulikuwa mkubwa lakini anashukuru kituo chao kuibuka washindi kutokana na juhudi wanayofanya katika kukuza bidhaa za Oryx pamoja na kutafuta masoko.

"Tunashukuru kwa kushinda na kupata tiketi kwa ajili ya kwenda Dubai ambapo tumelipiwa kila kitu kwa maana ya gharama zote, kwetu hii inatufanya tuongezee bidii zaidi kwa kuuza zaidi bidhaa bora za Oryx zikiwemo za Vilainishi vya magari,bodaboda na bajaji."

 Awali Arthur Awet ambaye ni B2C Key Account Manager Kampuni ya Oryx Services and Specialties Ltd amesema Oryx Services and Specialties LTD iliendesha shindano ya CODO na wasambazaji wao 50 ya kutafuta mtendaji bora wa mauzo katika bidhaa zao zote za vilainishi. 

"Leo ni siku ya makabidhiano ya tikiti kwa washindi, ambapo kila duka iliyoshinda imejishindia tiketi mbili ya Kwenda na kurudi Dubai ambayo gharama zote za safari zimelipwa. Safari ya washindi hawa itakua baada ya mwezi wa Ramadhan."



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025