HII HAPA KAULI YA FCC KUHUSU MATUMIZI YA AKILI MNEMBA



Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline

Tume ya ushindani (Fcc) imeomba serikali kupitia  mamlaka zake kuweka utaratibu wa kiudhibiti utakao wataka watoa  huduma kupitia mfumo  ya teknolojia kuweka bayana  changamoto zinazoweza kujitokeza kwa walaji wanapotumia teknolojia na namna wanavyoweza kuzitatua changamoto hizo.

Pia amezitaka Mamlaka za usimamizi wa soko ikiwemo FCC na Mamlaka nyingine zinazosimamia mifumo ya teknolojia kukaa pamoja na kujadili ili kuja na mapendekezo ya namna bora zaidi ya kusimamia eneo hilo.

Hayo ameyasema leo Mei 30 jijini Dar es salaam na  ,Mwenyekiti wa Tume ya  Ushindani (FCC), Dkt Aggrey Mlimuka wakati wa kongamano la matumizi ya akili mnemba yanayozingatia haki na uwajibikaji kwa mlaji   lililoenda sambamba na kauli mbiu isemayo 'Matumizi ya Akili mnemba yanayozingatia Haki na Uwajibikaji kwa Mlaji.


"Sote tuna shauku ya kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa ubora zaidi kwa walaji kwa kutumia teknolojia kama nyenzo muhimu kwa ustawi wa maslahi ya walaji na uchumi kwa ujumla lakini azma hiyo itakuwa na maana pale ambapo mifumo hii ya kiteknolojia itazingatia uwajibikaji, tija, haki na usawa kwa kuwekewa mifumo thabiti ya usimamizi na udhibiti "

Pia Mlimuka alisema kuwa matumizi ya akili mnemba katika huduma za malaji ni vyema  yabainishwe faida na athari  hasi ili kuwezesha watunga sera, sheria, mifumo ya usimamizi  na uthibiti pamoja na watafiti kuthibitisha faida na  hasara zilizopo na kuwezesha kubuniwa kwa taratibu zitakazohakikisha kuwa matumizi ya Akili Mnemba katika huduma za walaji yanazingatiwa misingi ya sheria, taratibu,  na kanuni za kumlinda mlaji na maslahi mapana ya mlaji.


"Walaji wana hofu namna ya mifumo huduma inayotumia akili mnemba namna inavyoundwa" amesema

Aidha alisema katika utekelezaji wa jukumu la msingi la kumlinda mlaji katika uchumi wa soko nchini Tanzania, amesihi kuundwa kwa mifumo ya  huduma inayotumia Akili Mnemba 

"Walaji wanahofu  kuhusu namba ambavyo mifumo huduma inayotumia Akili Mnemba inavyoundwa, tunapaswa kuhoji na kutafiti namna ambavyo mifumo hii inaundwa na kusimamiwa na endapo haya yanafanyika kwa namna inayolinda maslahi ya mlaji"

"Utafutaji na utumiaji wa taarifa za walaji ufanyike kwa ridhaa ya watumiaji, bila ulaghai  na taarifa hizo zisitumiwe vibaya" Alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa  Tume ya ushindani (FCC),  William Erio, alisema kongamano hilo limekutanisha waatalumu wa mifumo kutoka sekta za benki, usafirishaji pamoja na sekta nyingine za huduma ambao wataeleza ufahamu wao wa akili mlemba na kwa namna gani itakuwa inatumika duniani na katika nchi yetu.


Alisema kuwa wadau  hao watajadili kwa pamoja kuona namna gani wataweza kutekeleza haki za mlaji katika mazingira ya matumizi ya akili mlemba na kama kutakuwa na kikwazo cha kisheria hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kupitia taratibu za kiserikali na kuhakikiha matumizi ya akili mlemba yanatumika kisheria na walaji wanalidwa.

"Fcc kama taasisi iliyopewa jukumu la kumlinda mlaji inaweza ikawa na kanuni na sheria ambazo zinazingatia kumlinda mlaji wakati matumizi yanayofanyika ni ya akili mlemba" amesema urio

"Unapofanya  huduma za kupata usafiri  kama huba zile huduma zinapofanyika ni akili  mlemba, unapokata tiketi za ndege kinachofanya kazi ni akili mlemba, tuangalia kwenye upangaji wa bei kama inafanya haki kwa mlaji"











Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025