WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAOMBA KUIDHINISHIWA BAJETI YA SHILINGI 348,125,419,000 KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwc6xHCZ5DnRxyTPVFrLj4syRvdrVimuH7_KyPf3LaQSF9tQGqyDdci7J-SmqUeGrutqp3XYUJB8eArRmU2iVOxmRoIMhVJRKBi8XyQYgQydGW8f0VSl_hsf47YERX5tj-Kw0KBdIeHJI/s1600/IMG_ORG_1717175656559.jpeg)
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline Wizara ya Maliasili na Utalii imeomba kuidhinishiwa Bajeti ya jumla ya Shilingi Bilioni 348,125,419,000 (bilioni mia tatu arobaini na nane milioni mia moja ishirini na tano laki nne na elfu kumi na tisa) kwa matumizi ya Mwaka wa Fedha 2024/2025. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amesema hayo leo Mei 31/05/2024 wakati wa akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii Bungeni jijini Dodoma. Amesema kati ya fedha hizo zilizoombwa, Shilingi 250,884,083,000 (bilioni mia mbili hamsini milioni mia nane themanini na nne na elfu themanini na tatu) ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 97,241,336,000 (bilioni tisini na saba milioni mia mbili arobaini na moja laki tatu na elfu thelathini na sita) ni za Miradi ya Maendeleo. Fedha za Matumizi ya Kawaida zinajumuisha Shilingi 125,366,391,000 (bilioni mia moja ishirini na tano milioni mia tatu sitini na sita laki tatu na elfu tisini na moja) za Mishahara na Shilingi 125,517,6...