MWENYEKITI ADC ATANGAZA KUACHIA NGAZI ,KUGOMBEA URAIS 2025.
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Chama cha Allience For Democratic Change ADC Hamad Rashid Mohamed ametangaza kung'atuka rasmi kwenye nafasi ya mwenyekiti wa Chama hicho taifa huku akitoa raia Kwa wanachama kujitokeza kugombea.
Amesema Juni 27,mwaka huu Chama hicho kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu baada ya kukamilika Kwa chaguzi za ndani ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuutangazia umma hususani wanachama wa Chama hicho kwamba Yeye hatagombea tena nafasi hiyo badala yake Yuko tayari kugombea urais uchaguzi ujao kwasababu bado ana nguvu.
Hamad ameyasema hayo Leo Mei 29 ,2024 jijini Dar es Salaam katika Makao makuu ya Chama hicho Buguruni wilayani Ilala wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo pia amesema yupo tayari kugombea urais mwaka 2025 kupitia Zanzibar kama wanachama wataridhia.
"Chama hiki ni Chama ambacho kinafuata Demokrasia na Kuna utaratibu wa miaka kumi ya kukaa madaraka Kwa maana vipindi viwili vya miaka mitano na mimi tayari kama Mwenyekiti nimeshsongoza Kwa miaka 10 hivyo ni muda Sasa wa kuacha nafasi hii na kuwapisha wengine ."Amesema Kiongozi huyo ambaye ni gwiji kwenye siasa .
Nakuongeza ." Nitangaze rasmi kuwa Juni 27,2024 kutakuwa na mkutano wa uchaguzi mkuu ambao utafanyika hapa jijini Dar es salaam hivyo wananchi na hasa wanachama wa Chama chetu wajiandae kugombea kwani ADC ni Chama kinachofuata misingi ya Demokrasia ya kweli ."amesisitiza
Wakati huohuo Amesema chama chao kimetangaza kugombea nafasi ya ubunge visiwani Zanzibar ambapo tayari kimeshazindua kampeni zake na wamemsimamisha mwanamke kutokana na pia Chama hicho kinazingatia usawa katika nafasi za uongozi.
Uchaguzi mdogo wa ubunge umetokana na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo la Kwahani Ahamed Yahaya Abdulwakili (65) kufariki ghafla akiwa katika vikao vya bunge kule jijini Dodoma
Kwaupande wake katibu mku wa Chama hicho Doyo Hassan Doyo Amesema kuwa licha ya kung'atuka Kwa Mwenyekiti wo lakini bado kiongozi huyo atabaki kuwa Mlezi wa Chama hicho nafasi ambayo alikuwa nayo kabla ya kuwa hata Mwenyekiti wao.
Amesema Rashid Hamad ni kiongozi ambaye ameacha alama kubwa ndani ya chama cha ADC hivyo hakuna shaka kwamba atabaki kuwa kiongozi atakayekuwa na dhamana kubwa ya kuangalia vijana aliowaacha wanakwendaje
Pia akizungumzia kuhusu kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi ujao Amesema wanachama wataamua ila wao kama ADC wako tayari kuona nguli huyo wa siasa anakwenda kugombea urais akipeperusha bendera ya Chama hicho.
Comments
Post a Comment