ATE YAZINDUA TUZO YA MWAJIRI BORA WA MWAKA 2024
Na Mwandishi Wetu,DmNewsTz
CHAMA Cha Waajiri Tanzania -ATE kimezindua rasmi Tuzo ya Mwajiri Bora wa mwaka 2024 ambapo lengo la Tuzo hiyo ni
kuhamasisha Waajiri kuweka juhudi katika usimamizi wa rasilimali watu kwa kuweka misingi, kanuni na mikakati yenye mahusiano bora mahala pa kazi Ili kuwezesha kufanya biashara zenye Tija kwa taifa.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Leo Mtendaji Mkuu wa ATE Bi. Suzanne Ndomba amesema Mwaka huu vigezo vitatu vimeongezwa kwenye orodha ya tuzo zitakazoshindaniwa ambapo vigezo hivyo ni pamoja na Afya na Usalama pahala pakazi, Mwitikio dhidi ya VVU na Ukimwi na Utengenezaji wa Ajira.
Amesema katika kigezo Cha tuzo ya Mwitikio Dhidi ya VVU na Ukimwi lengo ni kuunga mkono juhudi na malengo ya serikali katika kupambana na maambukizi dhidi ya Ukimwi, kupinga unyanyapaa na vifo vitokanavyo na maambukizi ya Ukimwi.
Aidha ameeleza kwamba vipengele vya utoaji tuzo kwa Mwaka 2024 vitakuwa 17 ambavyo ni Ubora katika Usimamizi wa Rasilimali watu, tuzo yabutifautishwaji na ushirikishwaji, masuala ya utawala na Uongozi, ukuzaji wa vipaji, wajibu wa Taasisi kwa jamii na vinginevyo
Hata hivyo ametoa Rai kwa Waajiri wote wajitokeze kwa wingi kushiriki katika mchakato huu muhimu wa kumtafuta Mwajiri Bora wa Mwaka ambaye atatangazwa rasmi katika tukio kubwa la utoaji wa Tuzo hizi ambalo litafanyika Disemba mwaka huu.
Comments
Post a Comment