SAMIA AKAMILISHA AHADI MANYONI, KATIBU MKUU CCM DKT.NCHIMBI AKABIDHI.
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
MANYONI
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan leo Mei 29,2024 kupitia Katibu Mkuu wa chama hicho Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amekipatia chama wilaya ya Manyoni zaidi ya shilingi millioni 18 kwa ajili ya kuezeka jengo lake la kitega uchumi.
Katibu Nchimbi ameyasema hayo mbele ya Kamati ya Siasa ya Wilaya, mjini Manyoni, ikiwa ni mwanzoni mwa ziara yake ya siku mbili mkoani Singida.
Amesema fedha hizo zimetokana na ahadi ya Mwenyekiti ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Hassan Suluhu aliyoitoa kupitia kwa Katibu Mkuu wa zamani Daniel Chongolo.
Comments
Post a Comment