SUGU ASHINDA UWENYEKITI CHADEMA KANDA YA NYASA




Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline

Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ametangazwa Mshindi kwenye uchaguzi wa kumtafuta Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa ambapo amemuangusha aliyekuwa anatetea kiti hicho, Mchungaji Peter Msigwa.

Matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika leo May 29,2024 katika Mji wa Makambako Mkoani Njombe yametangazwa usiku huu baada ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa kupiga kura.

Sugu ameshinda kwa asilimia 51 huku Mchungaji Msigwa akipata asilimia 49 ya kura zilizopigwa.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Mshindi ni Frank Mwakajoka ambaye ni Mbunge wa zamani wa Tunduma.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025