WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAOMBA KUIDHINISHIWA BAJETI YA SHILINGI 348,125,419,000 KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025



Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline

Wizara ya Maliasili na Utalii imeomba kuidhinishiwa Bajeti ya jumla ya Shilingi Bilioni 348,125,419,000 (bilioni mia tatu arobaini na nane milioni mia moja ishirini na tano laki nne na elfu kumi na tisa) kwa matumizi ya Mwaka wa Fedha 2024/2025. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amesema hayo leo Mei 31/05/2024 wakati wa akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii Bungeni jijini Dodoma.

Amesema kati ya fedha hizo zilizoombwa, Shilingi 250,884,083,000 (bilioni mia mbili hamsini milioni mia nane themanini na nne na elfu themanini na tatu) ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 97,241,336,000 (bilioni tisini na saba milioni mia mbili arobaini na moja laki tatu na elfu thelathini na sita) ni za Miradi ya Maendeleo.

Fedha za Matumizi ya Kawaida zinajumuisha Shilingi 125,366,391,000 (bilioni mia moja ishirini na tano milioni mia tatu sitini na sita laki tatu na elfu tisini na moja) za Mishahara na Shilingi 125,517,692,000 (bilioni mia moja ishirini na tano milioni mia tano kumi na saba na laki sita na elfu tisini na mbili) za Matumizi Mengineyo. Fedha za Miradi ya Maendeleo zinajumuisha Shilingi 18,074,661,000 (bilioni kumi na nane milioni sabini na nne laki sita na elfu sitini na moja) fedha za ndani na Shilingi 79,166,675,000 (bilioni sabini na tisa milioni mia moja sitini na sita laki sita na elfu sabini na tano) fedha za nje.

Waziri Kairuki amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipa kipaumbele Sekta hiyo kwa kufanya uwekezaji mkubwa ambao umekuwa na matokeo chanya yenye mchango mkubwa katika kuimarisha uhifadhi, kuongeza watalii na mapato hivyo kuleta manufaa makubwa kwa uchumi wa Nchi yetu. 

Amesema pamoja na mafanikio mengi yaliyopatikana mafanikio matatu makubwa yaliyotokana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika Sekta ya Maliasili na Utalii chini ya uongozi wake mahiri ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watalii ambapo idadi ya watalii wa kimataifa imeongezeka kwa asilimia 96 kutoka watalii 922,692 Mwaka 2021




Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025