TIMU YA WIZARA YA MALISILI NA UTALII YATOA MISAADA KWA WAHITAJI ARUSHA



Na John Bera Dm,NewsOnline 
  ARUSHA

 TIMU  ya michezo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ikiongozwa na Mwenyekiti wa Timu hiyo, Getrude Kassara pamoja na viongozi mbalimbali wa Timu hiyo wamekabidhi  misaada ya hisani kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mei Mosi, Bi. Itika Mwankenja kwa ajili ya  kuipeleka kwa wahitaji  waliopo Mkoani Arusha ili iweze kuwasaidia.

Timu hii imedhihirisha ukarimu mkubwa kwa jamii kwa kuwasaidia watu wanaohitaji. Hatua hii ni mfano mzuri wa umoja na mshikamano katika kusaidia jamii kwa ujumla

Aidha, Wizara ya Maliasili na Utalii inajivunia kuwa na timu yenye moyo wa kujitolea ambayo  mbali na kuhamasisha utalii wa michezo pia, inarudisha kwa  jamii kwa namna moja au nyingine



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025