KAMPUNI YA ORYX GESI TANZANIA YAFANYA KUFURU KWA WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI ,WAGAWA MITUNGI YA GESI NA MAJIKO YAKE.




Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
 DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Oryx Gesi imekabidhi mitungi ya gesi ya kilo 15 na majiko yake Kwa wahariri ,waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya Mpango wake wa kuhamasisha matumisi ya Nishati safi ya Kupikia  Kwa watanzania

Akizungumza katika hafla fupi ya ugawaji wa mitungi hiyo  iliyofanyika Leo April 30 ,2024 Kwenye Kiwanda cha Kampuni kilichopo  wilayani kigamboni jijini Dar es salaam mkurugenzi mkuu BenoIte Araman Oryx Gas Tanzania wanauwezo wa kusambaza na kutoa Gas Tanzania bara na visiwani kwa wakati, muda wowote na sehem zote.

"Kwetu Oryx Gesi tukio hili tumelipa uzito mkubwa na hii inatokana na umuhimu wenu katika jamii yetu, kwetu sisi Oryx vyombo vya habari vimekuwa daraja na kiunganishi kikubwa cha kufikisha taarifa zinazohusiana na nishati safi ya kupikia na hasa inayotokana na gesi ya oryx kwa jamii."Amesema mkurugenzi Araman 

Nakuongeza kuwa "Sote tunafahamu Serikali yetu ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka kipaumbele katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia na Oryx Gas kwa kutambua umuhimu wa nishati safi tumeamua kuibeba kampeni hii kwa ukubwa wake"amesisitiza Araman.

Kwetu Oryx tukio hili tumelipa uzito mkubwa na hii inatokana na umuhimu wenu katika jamii yetu, nakwamba Oryx Gesi na kwenu vyombo vya habari imekuwa daraja na kiunganishi kikubwa cha kufikisha taarifa zinazohusiana na nishati safi ya kupikia na hasa inayotokana na gesi ya oryx kwa jamii"Amesema .

Mkurugenzi huyo mkuu Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt Samia Suluhu Hassan umeweka kipaumbele katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia na Oryx Gas kwa kutambua umuhimu wa nishati safi wameamua kuibeba kampeni hiyo kwa ukubwa wake.

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameeleza dhamira yake ni kuona ifikapo mwaka 2032 basi asilimia 80 ya Watanzania iwe inatumia nishati safi ya kupikia, Oryx Gas wamedhamiria kwa vitendo kufanikisha ndoto ya Rais 


Tumekuwa tukigawa mitungi ya gesi na majiko yake bure kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya baba na Mama Lishe,watumishi wa sekta ya afya na wajasiriamali.Tunayofuraha leo kukutana nanyi wahariri na waandishi wa habari katika tukio hilo la kuwakabidhi mtungi wa gesi wenye kilo 15 ukiwa na plate zake mbili.

Nakuongeza kuwa Kwetu tunakabidhi mitungi hii tukiamini ninyi ni kundi lenye ushawishi mkubwa hivyo mtasaidia kuhamasisha kwa vitendo jamii kuona haja ya kutumia nishati safi.

Mkurugenzi amehahidi kama ambavyo tumekuwa tukiahidi siku zote tutaendelea na kampeni hiyo kadri ya uwezo Wetu

Oryx Ges Tanzania mpaka sasa wameshatoa mitungi ya gesi zaidi ya 33,000 maeneo mbalimbali nchini na kiasi cha bilioni 1.5 kimeshatumika.
Kuna faida nyingi za kutumia nishati safi na hizi ni baadhi tu Kwa kutumia gesi ya Oryx kwenye taasisi mbalimbali, inasaidia kuongeza ufanisi katika uzalishaji na kupunguza muda wa taasisi husika kutafuta nishati nyingine kama kuni na mkaa.

Tukipika kwa kutumia Oryx Gas tunalinda mazingira yetu kwa kutokomeza ukataji wa miti, kwani misitu ni muhimu kwa kudumisha viumbe hai, kuhifadhi udongo, kusaidia mizunguko wa maji na pia uharibifu wa misitu ina haribu mifumo ya ekolojia na rasilimali za asili

Pia ina saidia kulinda afya ya wanawake ambao wanaathirika kwa moshi inayotokana na mkaa na kuni. Moshi una chembe chembe za sumu ambazo husababisha magonjwa kama pneumonia, cancer ya mapafu na matatizo ya upumuaji.

Akizungumzia faida za Gesi Amesema inaepusha wamama na watoto kuumia kwa kubeba kuni nzito na kuepuka kujeuriwa na Wanyama wakali wakiwa wanatafuta kuni. Na wanawake wataweza kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.




Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.