TMDA KANDA YA MAGHARIBI YAFANYA MSAKO WA KAMATA KAMATA DAWA HATARISHI.
Na Benny Kingson,DmNewsOnline
TABORA.
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa tiba kanda ya Magharibi TDMA Tabora imekamata dawa ya kuongeza nguvu za kiume aina ya Vega ambayo haijasajiliwa.
Pia mamlaka hiyo imekamata Sigara dawa kutoka India ambazo ubora wake haujulikani na zimeekwisha muda wa matumizi
Hayo yamebainishwa na Meneja wa TMDA Kanda hiyo Dkt .Christopher Migoha Machi 26,2024 katika mahojiano maalumu ofisini kwake na Mwandishi wa Habari hizi ambapo pia alitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai mwaka 2023 hadi Machi 2024.
Amesema katika kipindi hicho wameweza kukamata madawa yenye thamani ya sh.milioni 3,972,017.
Dkt Migoha amesema kati ya madawa hayo walikamata sigara dawa zenye thamani kubwa ya fedha ambapo miongoni mwa madawa hayo ni kutoka nchini India na kuongeza kuwa matumizi ya madawa hayo yana madhara makubwa kwa afya kwa kuwa yanaongeza msukumo wa damu mwilini.
“Madawa haya ni hatari kwa afya za jamii kwa kuwa yanamfanya mtumiaji awe na msukumo mkubwa wa damu mwilini,kitendo kinachoathili mfumo wa upumuaji na ubongo na kusababisha matatizo ya kisaikolojia na kufanya wakose kujiamini bila kuyatumia”amesema.
Meneja amesema katika kipindi hicho chote wamebaini madawa hayo hususani sigara dawa hizo zinatoka katia nchi za India,Burundi na Kongo ambapo nyingi ya sigara hizo wamezikuta zimemalizika muda wake wa matumizi lakini jamii imekuwa ikizinunua nakuzitumia.
Amesema kuwa kama wazalishaji wa bidhaa hizo wanahitaji kuendelea kufanya biashara,wanatakiwa kufuata utaratibu wa kuweka maandishi makubwa yanayoonyesha madhara yanayokana nayo kama ilivyo kwa bidhaa nyingine ili kuweka tahadhari kwa watumiaji.
Amesema katika ukaguzi huo wamekagua mifumo ya 30 ya mionzo ‘x-ray’,m-ray na’ utra sound’ ambapo walibaini mifumo 5 haifanyikazi na 25 peke ndiyo inayofanyakazi ikiwa ni sawa na asilimia 85 ambapo pia wamefanya ukaguzi wa maduka ya madawa 18 ya jumla,39 rejareja,kubaini maduka 10 yenye mifuko isiyoruhusiwa,maduka 400 ya dawa baridi,maduka 54 ya mifugo ,hospitali 37 na vituo 48 vya afya.
Dkt .Migoha amesema katika kipindi hichi wamefanikiwa kukusanya jumla ya sh.milioni 10 kupitia malengo yao 6 ya kudhibiti na 4 mtambuka udhibiti na kuhakikisha ufanisi wa vitendanishi na kwamba wana hudumia katika mikoa ya Tabora,Kigoma na Katavi.
Ameongeza kuwa wataendelea kuongeza nguvu zaidi katika kudhibiti,kutoa elimu na kuhakikisha watoa huduma wanafuata sherika,kanuni na miongozo pia kuwa wazalendo badala ya kujalai maslahi yao na kuhakikisha afya za jamii zinalindwa daima.
Amewataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa TDMA kwa kuwapa taarifa za wahusika wanafanya shughuli za kutoa huduma kinyume na maagizo ambapo watachukua hatua kali dhidi ya watakaobainika bila kujali wana umaarufu ama vyeo vikubwa.
Comments
Post a Comment