KATIBU MKUU WA CCM DKT. NCHIMBI AFIKA MSIBANI KWA MKE WA GACHUMA,TARIME NA KUTOA POLE.
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
TARIME
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amewasili wilayani Tarime, Mkoa wa Mara, kushiriki mazishi ya Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC), Jimbo la Mara Kaskazini, Francisca Mwita Gachuma.
Francisca ni mke wa wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, Christopher Mwita Gachuma
Dkt .Nchimbi baada ya kuwasili msibani nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Bomani, Tarime Mjini, leo Ijumaa, Machi 29, 2024, amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM.
Katibu Balozo Dkt Nchimbi ametoa pole Kwa wafiwa, wakiongozwa na Familia ya Mzee Gachuma, pamoja na kushiriki ratiba ya awali ya msiba, kabla ya mazishi yatakayofanyika Machi 30, 2024, huko Komaswa, Mjini Tarime
Comments
Post a Comment