VIONGOZI WA DINI WAOMBWA KUAMASISHA JAMII KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline 

VIONGOZI wa dini nchini wameombwa kushiriki kikamilifu katika kuimasisha jamii kuchana na uharibu wa mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia ili kuondokana na uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya kuni na mkaa katika kuandaa chakula.

Ombi hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi ya Oryx 1000 pamoja na majiko yake kwa viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali mkoani Kilimanjaro yaliyokwenda sambamba na utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya matumizi ya nishati safi ili kuepuka madhara kwa jamii.


Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema viongozi wa dini wanamchango mkubwa katika kusaidia jamii kutambua umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuachana kutumia kuni na mkaa.

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Shaban Fundi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Benoite Araman ametumia nafasi hiyo kueleza  kwa muda mrefu sasa wamekuwa wanajivunia kuwezesha makundi mbalimbali yakiwemo wanawake, watoto na wajasiriamali kupata nishati safi ya kupikia.


Amesema kwa kufanya hivyo wanaamini wanaikomboa jamii na taifa kwa ujumla wake kwani kupika kwa gesi ya Oryx kuna maanisha kuboresha afya za kinamama kwa kueuka kuvuta moshi mbaya wa kuni na mkaa.Pia tunaweza watoto kupata muda wa kwenda shule badala ya kutumwa kutafuta kuni,”amesema Fundi.

Aidha amekumbusha kuwa mwaka 2021 Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alianzisha kampeni ya nishati safi ya kupikia na alitoa maono yake ya kwamba ifikapo mwaka 2032  asilimia 80 ya wananchi itumie nishati safi, hivyo kuanzia hapo Oryx iliongeza nguvu na hadi sasa ya mitungi 19000 bure yenye thamani isiyopungua Sh.bilioni 1.5.


Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa dini ambao wamepatiwa mitungi ya gesi sambamba na kupatiwa mafunzo ya matumizi salama ya nishati hiyo, wamemshukuru mbunge Shally pamoja na Oryx kwa kutambua kundi hilo na nafasi yake katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia.




Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025