MIZIMU YA KATABI HIFADHI YA TAIFA KATAVI YAWAKIVUTIO KIKUBWA CHA UTALII.


Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
 KATAVI

IMEBAINISHWA  kuwa Hifadhi ya Taifa Katavi ni moja ya Hifadhi ambayo inavivutio vingi vya utalii ikiwepo kivutio kikubwa cha ziwa katavi ambalo limebarikiwa kuwa na viboko wengi sana ukilinganisha na maeneo mengine .

Hayo yamebainishwa februari 28 ,2024 na Afisa Uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa Katavi Beatrice Msuya wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wapo mkoani humo kwalengo la kuuzungumzia utalii wa hifadhi hiyo ya katavi.


Amesema kuwa Hifadhi ya taifa Katavi inasifika sana Kwa uwepo wa viboko wengi hasa kupitia ziwa katavi lakini  licha ya kusifika na kuwa na viboko wengi kupitia ziwa katavi lakini Kuna vivutio vingine Kama wanyama mbalimbali .

Beatrice ametaja  vivutio vingine ni uwepo wa Simba ambao wanatembea Kwa makundi, Twiga, Swara ,Tembo, Chuwi, Pundamilia, lakini Kuna aina mbalimbali za ndege.


Ameongeza kuwa Katika Hifadhi ya taifa katavi pia ina Uvuvi wa samaki Kwaajili tu ya .... na hakuna ruhusa ya kumla kwani wapo Kwaajili ya kivutio tu cha utali.

"Nawashauri watanzania kujenga utaratibu wa kudumu wa kutembelea vivutio vilivyopo katika Hifadhi yetu ya katavi na hasa nyakati  kama vile watoto wapo katika mapumziko ,nivema kuja kuona."Amesema 


Akizungumzia kuhusu historia ya mkoa wa Katavi ,Afisa UHIFADHI Beatrice Amesema jina la  katavi lilitokana na jina la Katabi ambaye alikuwa kama chifu na alikuwa anajishughuliaha mambo ya uwindani pamoja na kufanya matambiko mbalimbali ya kuomba mizimu Kwa lengo la kufanikisha jambo furani .

Amesema  Katabi alikuwa ni  kiongozi wa kimila katika mkoa huo ambapo jina lake la Katabi ndio umepatikana mkoa wa Katavi na Kwa wakati huo kulikuwa hakuna mtu ambaye alikuwa anaingia pasipo kupata kibari cha Katabi mwenyewe.


"Kimsingi Kwa histoa mkoa wa Katavi umetokana na mtu ambaye aliitwa Katabi ,na alikuwa ni kiongozi wa kimila na shughuli zake kubwa ilikuwa ni  uiwindaji na kufanya matambiko kupitia makabila ya wapimbwe na Wabende."Amesema 

Nakuongeza kuwa " mahala hapo ambapo palikuwa panafanyiwa matambiko pamekuwa ni sehamu ya kivutio cha utalii na Kwa makabila yanayozunguka Hifadhi hii na mkoa wa Katavi Kwa ujumla  bado wanaendelea kufanya ibada lakini Kwa kibari kutoka TANAPA ."Amesema 


Amewahamasisha watanzania kuja kutembelea Hifadhi hiyo ya taifa ya katavi ili kujionea vivutio vilivyopo lakini pia wageni kutoka nje ya Tanzania ikiwa pamoja na Afrika Mashariki kuja kutazama ukubwa wa hifadhi hiyo ambayo iliazishwa mwaka 1974.

"Ndugu zangu watanzania zile  nyakati za likizo njoo kwenye Hifadhi yetu ya katavi uje uone uzuri wake hakika utaona wanyama Kwa karibu na utajivunia kuwa sehemu ya  mtalii kupitia Hifadhi hii."Amesema .

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025