WAZIRI WA KAIRUKI ATOA MAAGIZO MAZITO KWA TANAPA, ALITAKA KUJA NA UBUNIFU WA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII.


Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline 
ARUSHA 

WAZIRI wa  Maliasili  na Utalii, Angellah Kairuki  ametoa maelekezo mazito  kwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kulitaka  libadilike ili liweze  kuchangia ipasavyo kwenye  uchumi wa taifa  kupitia utalii na kuhifadhi rasirimali  kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye.

Kairuki ametoa maelekezo hayo leo Januari 29,2024 kwenye hafla ya uvalishaji cheo na uapisho wa Kamishna  wa uhifadhi,Musa Kuji katika. Kwenye ofisi za  Makao  makuu ya TANAPA jijini Arusha.


Amesema kuwa  katika kipindi hiki Shirika la  TANAPA  linatakiwa kuja na  ubunifu wa hali ya  juu katika kutangaza vivutio vya utalii  na  kubaini mazao mapya  ya utalii ili sekta ya utalii iweze  kufikia lengo la Ilani  ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya  kuwa  na wageni  milioni tano na kuliingizia taifa jumla ya dola  za kimarekani bilioni sita ifikapo  mwaka 2025.

Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan kwa  maono yake ya kuifungua Tanzania  duniani kupitia Filamu ya The Royal Tour na kuwataka watumishi wa wizara  yake kuchapa kazi ili kuenzi  kwa vitendo  maono ya kiongozi huyo mkuu wa nchi .


Pia , ameitaka TANAPA  kukuza na kuimarisha mahusiano na jamii zinazozunguka  hifadhi na mbuga za taifa pia mahusiano na wadau mbalimbali wa  hifadhi na utalii ili kuweza kubadilishana  mawazo na uzoefu katika uhifadhi na kutangaza  vivutio mbalimbali vya utalii duniani pia uendeshaji wa Shirika kwa ujumla wake.

Ameongeza kuwa  katika kufanya kazi watumishi wanatakiwa kuzingatia kushirikiana na kufanya  kazi kama timu moja huku wakizingatia taratibu za Serikali  ili kuweza kupata matokea tarajiwa kwa haraka.


Kuhusu  utekelezaji wa miradi ya maendeleo Waziri Kairuki amesisitiza kutekeleza miradi yote kwa wakati huku akisisitiza  kufuata taratibu zote za manunuzi ya umma  kwa kuzingatia ubora na kuchukua  hatua  mapema wakati wowote inapotokea  changamoto  badala  ya kukaa kimya  na kuruhusu mitandao  kuendelea kupotosha.

Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas amemtaka Kamishna Kuji  kuwaunganisha watumishi  wote katika  kipindi chake  huku akimsisitiza kumtanguliza Mwenyezi  Mungu. 


Hafla hiyo ilipambwa na kikosi maalum cha wanamuziki kutoka TANAPA ambacho  kilitumbuiza wimbo maalum wa kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kucheza Filamu ya The Royal Tour.


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025