WAKULIMA WATAKIWA KUMUUNGA MKONO RAIS DKT SAMIA - MAJALIWA
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
RUANGWA
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka msisitizo katika kuendeleza Sekta ya kilimo kwenye mazao ya chakula na Biashara.
Amesema lengo ni kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa chakula na kila Mtanzania anayejishughulisha na kilimo aweze kukuza kipato chake na uchumi na taifa kwa ujumla.
Majaliwa ameyasema hayo leo Disemba 29,2023 wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Juhudi B kwenye kata ya Chinongwe, Ruangwa mkoani Lindi.
"Rais Dkt. Samia wakati wote amedhamiria kuhakikisha Tanzania inakuwa kimbilio la wengine wanaohitaji mazao “
Nakuongeza kuwa "Tumuunge mkono Rais wetu kwenye mapambano yake ya kukuza sekta ya kilimo, amefanya makubwa kwenye sekta ya kilimo ikiwemo kuagiza kutengwa kwa maeneo ya kilimo kwa ajili ya vijana”amesema Majiliwa
Comments
Post a Comment