RAIS DK.MWINYI AZINDUA UWANJA MPYA WA AMAAN COMPLEX

Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline

RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kujenga  uwanja mpya mwingine wa kisasa ambao utatumika katika mashindano ya AFCON mwaka 2027.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo akizindua rasmi Uwanja mpya wa Amaan Complex Desemba 27, 2023, Mkoa wa Mjini Magharibi. 

Pia Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali imelenga kujenga miundombinu ya michezo kila wilaya kwa viwanja vipya vya kisasa.



 Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Ujerumani kupitia shirika la maendeleo GIZ  imefunga mkataba wa makubaliano kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vitano vya michezo midogomidogo ikiwemo mpira wa kikapu, mpira wa wavu , mpira wa mikono na mpira wa pete.

Viwanja hivyo vinatarajiwa kujengwa Kangani Wilaya ya Mkoani, Mchangamdogo Wilaya ya Wete, Tumbatu na Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A na Haile Selasie Wilaya ya Mjini pamoja na viwanja vitatu vya Tennis Chakechake, Chuo kikuu cha SUZA Kampasi ya Nkurumah na Skuli ya Regeza Mwendo katika Wilaya ya Magharibi B.

Halikadhalika Serikali imefanikiwa kuwapeleka vijana katika nchi mbalimbali ikiwemo Uturuki na Afrika Kusini kwa lengo la kuendelezwa na baadae kucheza soka la kulipwa.

Rais Dk.Mwinyi amewahimiza wananchi kushiriki Tamasha la kila mwaka  la mazoezi linalofanyika tarehe Mosi ya mwaka mpya.



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025