Posts

WABUNGE ZAIDI 40 WASHIRIKI MKUTANO MKUU WA 14 WA AFRIKA WA JUKWAA LA UTAWALA WA MTANDAO

Image
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline               DAR ES SALAAM  NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ,Eng.Maryprisca Mahundi amefungua kikao Cha awali Jukwaa la Utawala wa Mtandao Barani Afrika. Akizungumza na waandishi wa habari Leo Mei 29,2025 Jijini Dar es Salaam amesema kwamba zaidi ya wabunge 40 toka nchi mbalimbali za Afrika wamehudhuria mkutano . Naibu Waziri Mahundi amesema kwamba kikao hicho ni maandalizi kuelekea ufunguzi rasmi wa mkutano unaotarajiwa kufunguliwa Mei 30,2025 unaohusu masuala ya Utawala wa Mtandao ambapo mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Aidha ,ameeleza kwamba serikali imejipanga kwa kuthibiti matumizi yasiyosahihi ya mitandao kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. "Wakati wa chaguzi mbalimbali wapo baadhi ya watu wanatumia vibaya mitandao hasa kudhalilisha wanawake kwahiyo wameonya kuwa hawatavumilia kwani sheria itac...

RAIS SAMIA APONGEZWA KUANZISHA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Image
                Na All an Kitwe, Tabora RAIS wa awamu ya 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kuanzisha mpango wa Bima ya Afya kwa wote hapa nchini kwa kuwa itawezesha wananchi kupata huduma bora za afya popote. Pongezi hizo zimetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Magharibi Dkt Emmanuel Lupilya alipokuwa akiongea na mwandishi wa gazeti hili juzi Ofisini kwake. Amesema kuwa mswada huo uliopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 1, 2023, ulipitishwa rasmi kuwa sheria mwaka 2024 baada ya kusainiwa na Mheshimiwa Dkt Rais Samia Suluhu Hassan. Amefafanua sheria hii itasaidia wananchi wote wa Tanzania Bara kupata huduma za matibabu kupitia mfumo wa Bima ya Afya kwa wote ambapo mwananchi atakuwa na uhuru wa kuchagua mtoa huduma yeyote wa Bima ya afya kumhudumia.  Dkt Lupilya ameeleza kuwa Bima hii ni muhimu sana kwa kuwa imelenga kuhakikisha kila Mtanza...

SHIRIKA LA AMEND LAZINDUA MIUNDOMBINU SALAMA KWA WANAFUNZI SHULE MAALUM SINZA .

Image
   Na Mwandishi Wetu,DmNewsonline                DAR ES SALAAM  NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) upande wa miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila amelipongeza Shirika la Amend pamoja na washirika wake kwa juhudi zao za kuhakikisha usalama barabarani kwa wanafunzi nchini Tanzania na barani Afrika na kusaidia kulinda maisha ya viongozi wa kizazi kijacho.   Akizungumza leo Mei 29, mwaka huu wakati wa hafla ya uzinduzi wa uboreshaji miundombinu salama kwa watoto shuleni iliyojengwa katika Shule ya Msingi Sinza maalum jiiini Dar es Salaam Mhandisi Mativila aliyemwakilisha Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa, amesema ni muhimu kuunga mkono mipango inayolenga kuwalinda watoto hasa wenye ulemavu na mahitaji maalum. “Nina matumaini mipango tunayoadhimisha leo itachangia mazingira salama kwa watoto wa shule hii ya Sinza Maalum na jamii kwa upana zaidi. Kwa kupunguza kasi ya vyombo vya moto, ...