Posts

SHIP CARS FOR LESS WITH EMIRATES SKYWARDS

Image
By Reporter, DmNewsOnline DUBAI Emirates Skywards has enhanced its Cash+Miles offering with select Emirates SkyCargo products that are tailor-made for transporting and treasured cars and beloved pets.  More than 2.4 million UAE based members can now use a combination of cash and Miles to lower shipment costs with Emirates Pets and Emirates Wheels. Skywards Miles can now be used towards the payment of outbound shipments made from the UAE only, with redemptions starting at 5,000 Miles.  Divisional Senior Vice President, Emirates Skywards, Dr Nejib Ben Khedher, Divisional Senior Vice President, Emirates Skywards, said: “At Emirates Skywards, we’re constantly looking for new ways to enhance our member offering and introduce new initiatives that unlock greater value, choice and flexibility.  Cash+Miles is one of our most popular initiatives and we’re thrilled to expand the offering to now include savings on select Emirates SkyCargo products, such as relocating beloved pets, or...

BoT YAJIZATITI KUIMARISHA MIFUMO YA UKUSANYAJI MAPATO

Image
Na Richard Mrusha,DmNewsOnline Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, amewataka Watanzania kuendelea kutumia huduma zinazotolewa na BoT kwa kuwa benki hiyo imeimarisha mifumo yake, hususan ile inayowezesha ukusanyaji wa mapato ya serikali. Tutuba ameyasema hayo siku ya Ijumaa Desemba 20, 2024 wakati ujumbe wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ulipofika katika ofisi za BoT kwa lengo la kuwapongeza na kutoa shukurani kwa Tutuba na watendaji wote walio chini ya taasisi anayoiongoza. "Kila mmoja ahakikishe anatumia mifumo iliyopo, mifumo yetu iko imara, madhubuti na haina changamoto zinazoweza kukwamisha ukusanyaji wa mapato", ameeleza Tutuba. Amesema BoT imejipanga vizuri kuhakikisha yeyote anayetaka kulipa analipa vyema kutokana na uwepo wa mifumo imara ambayo ipo chini ya idara mbalimbali za benki hiyo zinazowezesha ulipaji wa kodi kama Idara ya Benki, Idara ya Mifumo na Idara ya Mifumo ya Malipo. "Niwahakikishie kwamba akaunti zote za serikali zipo salama...

MBOWE ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UENYEKITI CHADEMA

Image
Na mwandishi wetu,DmNewsOnline DAR ES SALAAM  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ametangaza nia yake ya kugombea  nafasi ya uenyekiti wa chama hicho katika ngazi ya Taifa. Hayo ameyabainisha Disemba 21,2024 wakati akizungumza na  waandishi wa habari  Jjini Dar es Salaam, Mbowe amesema ametafakari kwa kina kuhusu kuachia nafasi ya uenyekiti huku akimkaribisha yeyote anayetaka kugombea kiti hicho. "Nimetafakari kwa kina sana. Nimesema mara nyingi nilitamani kuondoka, lakini siwezi kuondoka katikati ya minyukano iliyopo. CHADEMA nipo, nitakuwepo, nitagombea nafasi ya uenyekiti ngazi ya Taifa. Anayetaka kugombea, tukutane kwenye boksi.", amesema Mbowe. Mbowe  amekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kwa miaka mingi, amekuwa kipenzi cha wengi kutokana na msimamo wake wa kupigania demokrasia na haki za wananchi, licha ya changamoto kadhaa za kisiasa zinazokikumba chama hicho. Kwa upande mwingine, Tundu Lissu, ambaye ni mwanasiasa maarufu na...

SERIKALI YAKABIDHI NYUMBA 109 KWA WAATHIRIKA WA MAAFA HANANG

Image
Na mwandishi wetu,DmNewsOnline HANANG   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Ijumaa, Desemba 20, 2024) amekabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba, mwaka jana wilayani Hanang, mkoani Manyara. Akizungumza mara baada ya kukabidhi na kuzindua nyumba hizo zilizojengwa katika kitongoji cha Waret, Wilaya ya Hanang, mkoani Manyara, Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapa pole waathirika wote na amesisitiza kuwa Serikali itawasaidia ili waendelee na maisha yao kama ilivyokuwa awali.  Amesema kuwa ujenzi wa nyumba 73 kati ya 109 umegharamiwa na Serikali Kuu na kujengwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA-JKT); nyumba nyingine 35 zimejengwa na Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania, ilhali nyumba moja imejengwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UWT). “Kufuatia maafa hayo, nyumba 109 zilihitaji kujengwa upya kwa haraka. Hivyo, kwa kuzingatia athari hizo, na kwa upendo wake, ...

AIRTEL YATANGAZA PROMOSHENI YA MR.SANTA

Image
Na mwandishi wetu,DmNewsOnline DAR ES SALAAM  KAMPUNI   ya simu ya Mkononi  Airtel Tanzania katika msimu wa Sikukuu ya Christmass imekuja na zawadi kwa watumiaji wa mtandao huo kupitia promosheni inayoitwa MR. Santa. Mteja na mtumiaji wa mtandao wa Airtel  ili aweze kuingia kwenye kinyang'anyilo cha Mr. Santa anapaswa kufanya  miamala mbalimbali ikiwemo kutuma na kupokea pesa. Hayo yamebainishwa lDesemba 20,2024  Jijini Dar es Salaam na Meneja mahusiano wa Kampuni hiyo, Jackson Mmbando,  amesema droo ya promosheni hiyo itakuwa ikiwawezesha watumiaji wa mtandao huo kujipatia zawadi kem kem ikiwemo, fedha tasilimu na vitu vya thamani kama luninga, pikipiki , mbuzi , Smart fone za kijanja. " Hakikisheni wateja wetu wa  Airtel mnafanya miamala wiki hii kwa ajili ya Sikukuu ya Christmass kwa kutuma na kupokea pesa, kulipia bili mbalimbali utaweza kujishindia na kujipatia zawadi kutoka kwa mr. Santa," amesema Mmbando.  Aidha ameongeza kuwa mta...

NBAA YAIDHINISHA MATOKEO YA NOVEMBA 2024

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline DAR ES SALAAM BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeidhinisha matokeo ya mitihani ya 100 ya bodi hiyo iliyofanyika Novemba, 2024 ambapo ufaulu umeeongezeka kutoka asilimia 66.4 kwa mwaka uliyopita na kufikia asilimia 70.3 na wanaume wakiongoza kwa ufaulu wa mitihani hiyo. Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA. Pius A. Maneno imeeleza kuwa watahiniwa waliofanya mitihani hiyo walikuwa 6,908 sawa na asilimia 91.3 kati yao wanaume walikuwa 3,802 na wanawake walikuwa 3,764 huku watahiniwa 658 sawa na asilimia 8.7 hawakufanya mitihani kwa sababu mbalimbali. Aidha, kati ya watahiniwa 6,908 waliyofanya mitihani hiyo, watahiniwa 4,858 sawa na asilimia 70.3 wamefaulu mitihani yao ambapo watahiniwa 1,282 sawa na asilimia 18.6 wamefaulu masomo yote katika ngazi husika, hivyo wamestahili kupatiwa barua za ufaulu. Watahiniwa wengine 3,576 sawa na asilimia 51.7 wamefaulu...

MPANGO WA UTOAJI WA CHANJO NA UTAMBUZI WA MIFUGO KITAIFA KUANZA JANUARI 2025.

Image
Na Deborah Lemmubi, DmNewsOnline DODOMA WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Dkt Ashatu Kijaji ameeleza kuwa Serikali itaanza mpango wa utoaji wa chanjo na utambuzi wa Mifugo Kitaifa kuanzia Mwezi Januari 2025 ambapo Shilingi Bilioni 28.1 zimetengwa kwaajili ya kutekeleza  mpango huo unaolenga kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya mifugo hapa Nchini. Waziri Dkt Kijaji amesema hayo mapem leo hii Desemba 18,2024 Jijini Dodoma wakati akizindua Kampeni ya Chanjo za mifugo Kitaifa    Na kuongeza kuwa  mpango huo utakaotekelezwa kwa miaka mitano kutoka 2024-2029 na kugharimu Shilingi Bilioni 216 zitakazotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo Shilingi Bilioni 28.1 zitatumika awamu ya kwanza ya uchanjaji na utambuzi wa mifugo kuanzia Mwezi Januari 2025. "Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeridhia kugharamia mpango wa chanjo wa miaka mitano kuanzia mwaka 2024 hadi 2029 wenye thamani ya Shili...