Posts

RAIS SAMIA NI CHAGUO LA MUNGU - ASKOFU SHOO

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline Askofu Dkt. Frederick Shoo ameeleza kwa uzito kuwa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ni ishara thabiti kuwa wanawake wana uwezo sawa wa kuongoza, akimtaja kama mfano wa kimungu wa kuwatia moyo Watanzania. Alihimiza jamii kuachana na dhana potofu za kijinsia na kuwatazama wanawake kama viongozi waadilifu na wenye uwezo katika jamii na kanisa. Aidha, Askofu Shoo ametoa kauli ambayo wengi huinong’ona lakini wachache huisema wazi—kwamba baadhi ya ukosoaji dhidi ya Rais Samia unatokana na jinsia yake, ikizingatiwa jamii yetu ya kihafidhina ambayo haijazoea kiongozi mwanamke. Watanzania wanapaswa kutafakari maneno ya Warumi 13:1: *"Kila mtu na atiye mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo imewekwa na Mungu."* Kwa mafanikio ya uongozi wake ndani ya muda mfupi, ni dhahiri kuwa Mungu yuko pamoja naye na anamtumia kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.

MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI AMETOA UFAFANUZI KUHUSIANA UPOTOSHAJI WA TAKWIMU ZA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022 UNAOENDELEA KWA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI HUSUSANI MITANDAO YA KIJAMII

Image
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline DAR ES SALAAM   MTAKWIMU Mkuu wa   Serikali Dkt.Albina Chuwa ametoa ufafanuzi kuhusiana na upotoshaji wa Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 unaoendelea kufanyika kwenye baadhi ya vyombo vya habari hususani mitandao ya kijamii. Hayo ameyabainisha Oktoba 28,2024 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa kwa mujibu wa Kifungu Cha 6 Cha Sheria ya Takwimu SURA 351 kinamtaka Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoa ufafanuzi wa tafsiri sahihi ya takwimu zinazotolewa au zinazopotoshwa kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Aidha,Kanuni za Msingi za Umoja wa Mataifa Kuhusu Takwimu Rasmi(United Nations Fondamental Principles of Official Statistics),Kanuni Na.4 ambayo inaeleza"Ofisi za Takwimu zinahaki na wajibu wa kutoa ufafanuzi juu ya tafsi potofu na matumizi mabaya ya takwimu rasmi".amesema Dkt.Chuwa amesema kwamba Serikali kupitia Waziti wa Nchi,Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikalo za Mitaa (TAMISEMI)....

MWENYEKITI CCM PICHA YA NDEGE AWATAKA WANACHAMA KUVUNJA MAKUNDI

Image
Na Victor Masangu,DmNewOnline  KIBAHA  MWENYEKITI  wa Chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Picha ya ndege iliyopo katika Halmashauri ya Kibaha mji Grace Jungulu amewahimiza wanachama wote kuhakikisha kwa sasa wanavunja makundi yote na kuungana kwa pamoja na kueleleza nguvu ili kushinda kwa kishindo  katika uchaguzi wa serikali za mtaa. Jungulu ameyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya viongozi na wanachama wa ccm ikiwa ni baada ya kumalizika kwa zoezi la kura la maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea ambao watakiwakilisha chama katika uchaguzi huo. Amesema kwamba mchakato wa kura za maoni umeshafanyika na kumalizika  hivyo.mgombea ambaye atakwenda kukiwakilisha  chama wa CCM inapaswa apewe ushirikiano wa kutosha na kuweka kabisa tofauti ambazo zilikuwepo hapo awali kwani wote lengo ni moja katika kukijenga na kikiimarisha  chama. "Kwa kweli mimi ninashukuru Mungu kama Mwenyekiti tumeweza kushirikiana bega kwa bega na wana ccm wenzangu tangu hatua za aw...

MLAWA APONGEZA KAMPENI YA 'TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIKIWA' ATIA NENO.

Image
Na Eliasa Ally,DmNewsOnline IRINGA  MDAU wa Maendeleo kutoka wilaya ya kilolo Mkoa wa Iringa Aidan Mlawa ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya john Galt Hauliers LTD ya Usafirihaji wa Mizigo ndani nje ya Tanzania amepongeza kampeni ya 'Tuwambie kabla Hawajaharibikiwa' iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba ikilenga kutoa Elimu kuhusu ukatili wa kijinsia Mkoani hapo. Mlawa amesema anategemea kuzinduliwa kwa kampeni hiyo kutasaidi kupunguza matukio ya ukatili dhidi ya watoto ambao ni wahanga wakubwa wa  matukio haya ndani ya Mkoa wa Iringa. "Mkoa wetu umekuwa na matukio mengi ya ukatili hasa ubakaji na ulawiti kwa watoto zetu niombe kampeni hii tuibebe tuwe marafiki kwa vijana wetu tuwaelimishe ili wawe wanatoa taarifa wanapokumbwa na ukatili bila kutuogopa" Alisema Mlawa  Mlawa ameongeza kwa kuwaasa wazazi kutowaficha ndugu kwa kigezo cha uhusiano pale wanapotenda makosa ya namna hiyo. "Kumekuwa na wazazi na walezi ambao wanawaficha ndugu zao wa...

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline 1. Kupoteza Ushawishi kwa Umma: Chama Cha Chadema kimekosa mvuto kutokana na kukimbiwa na wanasiasa wenye uwezo wa kushawishi, wanasheria mahiri, na wanataaluma wakubwa. Wakati zamani walijenga hoja na ajenda zenye nguvu, sasa wamesalia bila nguvu ya kushawishi umma. 2. Migogoro ya Viongozi wa Juu: Mgawanyiko na chuki baina ya viongozi wakuu kama Freeman Mbowe na Tundu Lissu kwa ajili ya nafasi ya urais ni ishara ya ukosefu wa umoja. Migogoro hii inavuruga utendaji na kuashiria kukosekana kwa mshikamano. 3. Chaguzi za Ndani Zenye Matabaka: Mfumo mpya wa usajili "Chadema Digital" umeweka kipaumbele kwa wenye nacho, hivyo kupunguza uaminifu wa chama kwa masikini na kuwagawa wanachama kulingana na uwezo wao kifedha. Je, chama kinachodai kusimama na maskini kinauza kadi kwa milioni moja kwa wanachama wake? 4. Rushwa Inayotawala Chama: Viongozi wa Chadema wanahusishwa na rushwa, kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa hadi rushwa ya ngono katika nafasi za...

MAJALIWA : WATANZANIA TULINDE UTAMADUNI WETU KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO

Image
Na mwandishi wetu,DmNewsOnline DAR ES SALAAM    WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wahakikishe wanalinda utamaduni na kujenga misingi ya kuhamasisha vijana na vizazi vijavyo kutambua na kuenzi historia na urithi wa Mtanzania. Amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kutunza utamaduni, mila na desturi kwa sababu utamaduni ni nguzo ya utambulisho wa jamii husika na ni muhimu kwa kizazi kijacho. Amesema hayo leo (Jumapili, Oktoba 27, 2024) wakati akifungua Tamasha la Buhaya 2024 ‘Buhaya Festival’ lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. “Katika siku za sasa, ambapo teknolojia na utandawazi vinazidi kuimarika, ni rahisi kupoteza mila na desturi zetu, hivyo tunaposhiriki tamasha hili, tunajifunza na kuhamasisha jamii zetu kuhusu umuhimu wa urithi wetu wa kiutamaduni.” Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewaasa wazazi, jamii na madhehebu ya dini kuendelea kuhimiza utunzaji wa maadili kwa kuzingatia mila na desturi ili kuepuka mmomonyoko wa maadil...

USHIRIKI WA LISSU KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA WAZUA GUMZO

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline Wakati Watanzania wanajiandaa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, ambao ni nyenzo muhimu kwa wananchi kushiriki kwenye mchakato wa maendeleo ya kijamii, maswali makubwa yanaibukakuhusu Chadema na viongozi wake.  Katika kipindi ambacho chama kinatakiwa kuwa mstari wa mbele, mmoja wa viongozi wakuu, Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu, hayupo nchini na hajajisajili hata kupiga kura.  Tundu Lissu, akiwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, ana wajibu wa kuwaunganisha wafuasi wake, kuwapa mwongozo, na kuwahamasisha kushiriki katika uchaguzi.  Hata hivyo, kwa kushangaza, Lissu amekaa nje ya nchi katika kipindi hiki muhimu.  Kutojisajili kwake kupiga kura kunazua maswali juu ya dhamira yake na uaminifu wake kwa wafuasi wa Chadema na Watanzania kwa ujumla. Wafuasi wanahitaji kuona viongozi wao wakiwa tayari na wenye dhamira ya kushiriki kikamilifu.  Pia Kutokuwepo kwa Lissu kunatuma ujumbe ambao unaweza kuchukuliwa vibaya na wafuasi na kupunguza imani ...