TAKUKURU TEMEKE YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUMISHI KWA WIZI WA TSH.169,617,529

 Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline

        DAR ES SALAAM 

TAASISI ya Kupambana na Rushwa Mkoa wa Temeke(TAKUKURU) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mashtaka,imewafikisha Mahakamani watumishi wa Halmashauri  hiyo na OR-TAMISEMI kwa tuhuma za wizi na ubadhirifu wa fedha kiasi cha shilingi 169,617,520 maarufu kama Fedha za BAKAA.

Akizungumza na waandishi wa habari Juni 2,2026  Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Temeke, Fransis Luena amesema watumishi waliofikishwa  mahakamani kwa makosa hayo kutoka OR-TAMISEMI DODOMA ni Annie Maugo-Afisa Hesabu Mwandamizi,Tumsifu Kachira-Afisa Hesabu Mwandamizi Daraja la na Aidan Mponzi-Afisa Hesabu Daraja la 1.

Aidha ,amesema watumishi wengine  kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ,Jonathan Manguli-Afisa Hesabu 1 na (MUSE),Godfrey Martiny-Mkuu wa Kitengo Cha Fedha na Uhasibu,Juvenalis Mauna-Mkuu wa Kitengo Cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira,Josephat Mutembei-Mhandisi,Bibiana Mdete-Mtunza Bohari na Henry Rugayi-Afisa Ugavi pamoja na wafanyabiashara ,Hamis Manfred-Mkurugenzi Mtendaji Konya Investment Co.Ltd,Paul Mwakyusa-Mmiliki wa Mbogholo Investment Co.Ltd na Godwin Cheyo-Mmiliki wa Macheye Tz Investment.

"Washitakiwa watatu Juvenalis Mauna,Josephat Mutembei naHamis Manfred wamekiri makosa kupitia makubaliano(plea-bargain) na wamesharejesha jumla ya shilingi 87,000,000/ = na kulipa faini ya shilingi 3,500,000/= ambapo Juvenalis Mauna amerejesha shs.27,000,000/= na faini shs.2,000,000/=,Hamis Manfred amerejesha shs.40,000,000/= faini ya 1,500,000/= na Josephat Mutembei amerejesha 20,000,000 na washtakiwa wengine 9 shauri lao linaendelea mahakamani",amesema

Pia ameeleza kuwa TAKUKURU Temeke ilifuatilia matumizi ya jumla ya shilingi 6,532,990,529 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 7 ya maendeleo katika  sekta za elimu,afya na 
ujenzi inayotekelezwa na Halmashauri za Manispaa ya Temeke na Kigamboni.

Katika taarifa hiyo ya utekelezaji TAKUKURU Temeke imefanikiwa kuongeza uelewa  kwa kutoa elimu kwa wananchi 20804 kupitia mikutano 8,maonesho 3,semina 6,uimarishaji wa klabu 30 za wapinga rushwa katika shule za msingi,sekondari na vyuo pamoja na kipindi kimoja cha redio.

Kwa kipindi Cha Januari Hadi Machi 2026 TAKUKURU Temeke  imefanikiwa kuokoa na kurejesha shilingi 370,000/= kwa madereva Bajaji 40 wa kituo Cha Kibada-Kigamboni waliokuwa wakitozwa fedha kwa njia isiyo halali wakidaiwa kulipia sticker za maegesho na wamefanikiwa kurejesha fedha hizo kwa wahusika pamoja na kuimarisha utulivu na Imani katika kituo hicho.

"Katika robo ya Januari-Machi ,TAKUKURU imepokea malalamiko 68,ikiwa ni ongezeko la asilimia 42.7% ikilinganishwa na robo iliyopita,Hali inayoashiria kuimarisha Kwa Imani ya wananchi wa utayari wa kuripoti vitendo vya rushwa",amesema

Hata hivyo,TAKUKURU Mkoa wa Temeke imejipanga kuendelea kutekeleza mikakati ifuatayo kwa kuimarisha shughulu za uchunguzi kwa kutoa kipaumbele Cha juu kwa malalamiko yote yanayohusu rushwa,kuzingatia mwenendo wa takwimu za vipindi vilivyopita.Mpango mkakati unalenga kuongeza Kasi na ubora wa uchunguzi,kukamilishamashauri kwa wakati na kuhakikisha kesi zenye ushahidi wa kutosha zinafikishwa mahakamani.

Sanjari na hayo pia wameweka maazimio na mapendekezo katika vikao kati ya TAKUKURU na wadau mbalimbali katika kuhakikisha hatua zinazopendkezwa kupitia uchambuzi wa mifumo inatekelezwa ilikuziba mianya ya rushwa,kuimarisha uwazi na kuongeza uwajibikaji. 

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.