Posts

Showing posts from February, 2026

KUNDI LA 11 LAMPANGO WA FFP LAKABIDHI HUNDI YA MILIONI 30 KWA JKCI

Image
Na mwandishi wetu,DmNewsTz Dar es salaam  Kundi la 11 la Mpango wa Female Future Programme (FFP) limekabidhi hundi ya shilingi milioni 30 kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) kwa ajili ya kusaidia watoto wanaokabiliwa na matatizo ya moyo. Mchango huo umetolewa kama sehemu ya shughuli za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) za darasa la washiriki 162 wa mwaka 2025, ambalo ni darasa kubwa zaidi kuwahi kushiriki katika historia ya mpango huo unaoratibiwa na Association of Tanzania Employers (ATE). Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mtendaji Mkuu wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba-Doran, amesema kuwa Mpango wa Female Future Programme haujikita tu katika utoaji wa mafunzo bali pia unalenga kuwajengea wanawake viongozi uwezo wa kuchukua hatua chanya katika jamii. Alisema hadi sasa jumla ya wanawake 620 wamehitimu kupitia mpango huo. Alifafanua kuwa utekelezaji wa mradi wa CSR ni sehemu ya mafunzo ya kukuza ujuzi wa uongozi wa juu ambayo washiriki wa Kundi la 11 wamepa...

JAMII YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA POLISI KUFICHUA UHALIFU.

Image
  Na Eliasa  Ally,DmNewsonline                     IRINGA     KAMANDA  wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, ameitaka jamii kuacha tabia ya kuficha wahalifu na badala yake kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mapema ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza. Kamanda Bukumbi ametoa wito huo Februari 27, 2026  akisisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi ni nguzo muhimu katika kupambana na vitendo vya uhalifu na kudumisha usalama wa jamii. Aidha, Kamanda Bukumbi anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara kesho Februari 28, katika uwanja wa Shule ya Msingi Mawelewele, Kata ya Mwangata.  Lengo la mkutano huo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mapambano dhidi ya uhalifu pamoja na kusikiliza changamoto zao ili kuimarisha usalama na ulinzi wa raia na mali zao. Jamii inahimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mkutano huo muhimu. 

PROF. SHEMDOE ATAKA MAGEUZI YA UCHUMI WA VIJIJINI KUHUSISHA UCHUMI WA BULUU, UFUGAJI, MISITU NA MAZAO YAKE

Image
Na Mwandishi wetu, DmNewsOnline Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema ili mageuzi ya uchumi wa vijijini yawe na tija na manufaa kwa wananchi yanapaswa kuhusisha  uchumi wa buluu, ufugaji pamoja na misitu na mazao yake. Prof. Shemdoe amesema hayo  Februari 26, 2026 wakati akichangia mada juu ya mageuzi ya uchumi na maendeleo vijijini kwenye mkutano wa pili wa Kimataifa wa Mageuzi ya Uchumi na Maendeleo Vijijini unaoendelea katika mji wa Cartagena, nchini Colombia, akimwakilisha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo. Mchango huo wa Prof. Shemdoe umelenga kutimiza azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukifanya kilimo na ufugaji kuwa na faida kwa wananchi na sio shughuli za kujikimu, kukuza uchumi wa bluu kwa kutumia rasilimali za maji kuongeza kipato cha jamii za Pwani, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi na kutumia misitu kwa njia endelevu ili kuongeza thamani ya mazao yake na kulinda mazingira. Katika kikao cha kuja...

TPSF YAIOMBA SERIKALI KUJADILI MABADILIKO YA KISERA YA KIKODI.

Image
  Timothy Marko DmNews Online.               DAR ES SALAAM TAASISI ya Sekta Binafsi Nchini Tanzania (TPSF)imeomba Wizara ya Fedha kuweza kukaa na taasisi hiyo ili kuweza kufanya mapitio  ya sera ya kodi ilikuweza kuchochea Mazingira Wezeshi ya ufanyaji Biashara.  Akizungumza Leo Febuari 27,2026 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Sera na Utafiti Taasi hiyo  Mwanahamis  Hussein amesema kuwa lengo kubwa la kutaka kukutana na Wizara ya Fedha ni pamoja na  kujadilianaSera mbalimbali za kifedha. "Tunataka kupeleka Mapitio haya sera kabla ya Bunge la Bajeti"Amesema Mkurugenzi wa Sera na Utafiti TPSF  Mwanahamis  Hussein.  Mwahamis Ameongeza kuwa lengo nikutaka Mabadiliko ya Sera za kodi katika sekta ya Viwanda na Madini ili kuweza kuchochea Uchumi Nchini.  Amesisitiza kuwa Kikao hicho kitatoa Dira na mwelekeo wa hali ya ukuaji wa Biashara Nchini na kuweza kuchangia pato la taifa.

POLISI IRINGA WATOA WITO WA MSAADA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WA MAUAJI YA BENITO

Image
  Na Eliasa Ally Iringa,DmNewsonline                          IRINGA  JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa limewaomba wananchi kushirikiana nalo kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa watuhumiwa wa mauaji ya Benito Avinashi, mkazi wa Wanipogolo, huku likikanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu kupotea kwa baadhi ya watuhumiwa  Akizungumza na waandishi wa habari,   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Alan Bukumbi, amesema kumekuwa na taarifa zisizo sahihi katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa Ibrahim Myovela , Asajile Antony, Antony Mwaisaka  na Aly Kalolo wamepotea mikononi mwa Polisi ìringa Kamanda Bukumbi amefafanua kuwa watuhumiwa hao wanatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma mbalimbali za jinai, ikiwemo kuvunja masharti ya dhamana pamoja na kuhusishwa na makosa ya uchochezi kupitia mitandao ya kijamii. Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, katika hatua za awali za uchunguzi, mtuhumiwa...

MWENYEKITI ACT _WAZALENDO NGOME YA VIJANA WANAWAKE KUSHEHEREKEA SIKU HIYO KWA KUTEMBELEA WATOTO YATIMA

Image
  Timothy Marko DmNews Online              DAR ES SALAAM.  MWENYEKITI Ngome ya Wanawake Taifa wa Chama Cha ACT Wazalendo Janet Rite amewataka Wanawake Nchini kusherekea Siku hiyo kwa kutembelea watoto yatima. Akizungumza Leo Febuari 26,jijini Dar es Salaam Janeth Rite amesema kuwa Siku hiyo itumike kuona yatima na kuwafariji. Amesema kuwa Chama hicho kitatumia Marchi 8 ambayo ni siku ya Wanawake kwenda kuwa fariji yatima waliopoteza Wazazi wao  sambamba na kufanya Usafi Hospitalini. "Tutatoa Damu ilikuweza kuokoa Maisha  ya watanzania,Tutatembelea Makaburi yawaliofariki October 29,2025." Amebainisha Janet.  

MIRADI YA HALMASHURI YA JIJI LA DAR IMEKAMILIKA KWA ASILIMIA 89_Dc MPOGOLO

Image
  Na Angelina Mganga,DmNewsOnline            DAR ES SALAAM  MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambapo taarifa hiyo imejikita katika kipindi cha miaka minne ya Julai mpaka Desemba 2025. Akiwasilisha taarifa hiyo Leo Februari 25,2026 Jijini Dar es Salaam DC Mpogolo amesema taarifa hiyo imejikita katika kipindi Cha miaka 4 ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na tunamshukuru Rais kwa kutoa fedha nyingi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam . Aidha amesema miradi mingi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekamilika kwa asilimia 89. DC Mpogolo ameeleza kuwa katika Wilaya ya Ilala ina wanafunzi zaidi ya laki nne kwa shule ya msingi na Sekondari na changamoto kubwa ni vyumba vya madarasa lakini Halmashauri imejikita katika upatikanaji wa vyumba na kuhakikisha inajenga  vyumba kwa ajili ya wanafunzi kwa elimu msingi na elimu sekondari pamoja na madawati ...

PROF. SHEMDOE AONGOZA UJUMBE KUMWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA KILIMO, ARDHI NA MAENDELEO VIJIJINI, COLOMBIA

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline Colombia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa wa nchi zinazoshughulika  na masuala Kilimo, Ardhi na Maendeleo vijijini,  ulioanza  Februari 24, 2026 nchini Colombia kwenye jiji la Cartegina. Prof. Shemdoe amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo, baada ya Mhe. Rais kupokea mwaliko wa kuudhuria mkutano huo kutoka kwa Rais Gustavo Petro Urrego wa Colombia.  Lengo kuu la mkutano huo uliohudhuriwa na nchi zaidi 100 duniani, ni kutoka na mwafaka wa namna gani matumizi bora ya ardhi katika kilimo yanaweza kupunguza migogoro ya ardhi na kuharakisha maendeleo vijijini. Aidha nchi hizo zaidi ya 100 zilizoshiriki mkutano huo, ambazo zinashughulika na masuala ya Kilimo, Ardhi na Maendeleo ya Vijijini, zimepata fursa ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya kilimo, Ardhi na Maendele...

JESHI LA POLISI DAR LIMEWAKAMATA WATUHUMIWA 46 KWA WIZI

Image
  Na Angelina Mganga,DmNewsOnline        DAR ES SALAAM  JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limewatia mbaroni  watu wapatao 46 kwa tuhuma za makosa ya kijinai ikiwemo,unyang'anyi wa  kutumia nguvu, kuvunja nyumba na maghala(Godown)pamoja na wizi  wa mali mbalimbali. Akizungumza  na waandishi wa habari  Februari 24,206  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam SACP Jumanne Muliro amesema  watuhumiwa hao wamekamatwa katika kipindi cha kuanzia Januari 30 hadi Februari 24, 2026. Aidha,Kamanda Muliro amebainisha   kuwa baadhi ya watuhumiwa hao walikuwa wakitumia pikipiki na silaha za jadi kama vile mapanga kutekeleza uhalifu huo,hususan maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es salaam. Amesema kuwa wapo watuhumiwa waliokuwa wakijihusisha na kuvunja nyumba mchana na usiku na kuiba vifaa mbalimbali,huku wengine wakihusika na kununua na kuuza mali za wizi. "Jeshi la polisi limekamata pikipiki zaidi ya 20(...

NSVINGA AIPONGEZA SEKTA YA MADINI

Image
  Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline            DAR ES SALAAM  MKURUGENZI wa Kampuni ya Nation Laboratory,Happiness Nsvinga ameipongeza sekta ya Madini kwa kufanikisha makubaliano na Benki ya CRDB kwa lengo la kuwawezeaha wachimbaji kupata mitaji kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao. Akizungumza kuhusu makubaliano hayo,Nsvinga amesema  upatikanaji wa mtaji umekuwa changamoto kubwa kwa wachimbaji wengi,hasa wadogo,na kwamba kufanya biashara ya madini jambo gumu.Ameeleza kuwa hatua hiyo inafungua ukurasa mpya kwa wachimbaji kwa kuwawezesha kupata fedha zitakazowaongezea uwezo wa uzalishaji wa kukuza biashara zao. Amesisitiza kuwa kwa pamoja na umuhimu wa mtaji na maarifa,kipengele muhimu zaidi katika biashara ya madini ni kufanya vipimo sahihi vya madini. Amesema bila vipimo ya uhakika hata kama mfanyabiashara na mtaji na uzoefu atakosa mwelekeo sahihi. Nsvinga amewahimiza wadau wote wa biashara ya madini kuhakikisha wanafanya vipimo katika maabara...