WATANZANIA MSIKUBALI KUYUMBISHWA KUINGIZWA KATIKA MACHAFUKO’
Mwandishi wetu,DmNewsonline WATANZANIA wameshauriwa wasikubali kuyumbishwa na wanaharakati ambao wenyewe wapo kwa ajili ya kuiona nchi ya Tanzania inavurugika na kukosa utulivu. Ushauri huo umetolewa leo Novemba 30 ,2025 jijini Dar es salaam na wanaharakati huru ambao wamemua kueleza hatua kwa hatua mbinu chafu ambazo zinatumiwa na baadhi ya wanaharakati ambao wamekuwa wakitafuta mbinu mbalimbali kuvuruga amani ya Tanzania. Wamesema kuwa sababu kubwa ya vurugu ambazo zinatengenezwa na wanaharakati hao wenye nia ovu na Taifa la Tanzania ni kutaka kuvuruga kasi ya ukuaji wa maendeleeo ambayo imekuwa tishio kwa baadhi ya nchi jirani. Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Mwanaharakati Huru Ahmed Kombo amebainisha kuwa tangu kuazishwa kwa vyama vingi nchini mwaka 1995 baadhi ya wanaharakati na vyama vya siasa vya upinzani vimekuwa vikilalamikia tawala zote ambazo zinapita katika uongozi wa nchi yetu. Amesema kuazia utawala wa Awamu ya Tatu ch...