TLP KINAWATA WANACHAMA WENYE SIFA KUJITOKEZA KWA WINGI KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI

Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline . DAR ES SALAAM CHAMA cha Tanzania Labour Party(TLP) kinapenda kuwataarifu na kuwatangazia wanachama wote pamoja na wananchi na wapiga kura kuwa kimeanza kutoa fomu za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Ubunge na Udiwani kuanzia Aprili 25,2025. Akizungumza na mwandishi wa habari wa DmNewsOnline kwa mahojiano maalum Ofisi kwake leo Aprili 30,2025 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa TLP Taifa,Richard Lyimo amesema kwamba fomu za Urais zinapatikana Makao Makuu ya Chama Dar es Salaam na Ofisi ndogo za Zanzibar na zoezi la kuchukua fomu lilianza Aprili 25,2025 na mwisho ni Mei 15,2025 kwa wagombea wa Urais. Aidha,Mwenyekiti Lyimo amesema kuwa fomu za Ubunge na Udiwani zinapatikana kwenye ofisi zetu za Mikoa,Wilaya na Majimbo kwa nchi nzima kwa wenyeviti wa Mikoa,Wilaya,Majimbo na Makatibu na zimeanza kutolewa Aprili 30,2025 hadi...